RUKWA: WAZIRI UMMY AWAONYA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WASIOTENGA FEDHA ZA UWEZESHAJI WANAWAKE

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaonya Wakurugenzi wote wa Halmashauri wtakaokaidi agizo la Serikali la kutenga asilimia 4 kwa  ajili ya wanawake na vijana pamoja na asilimia 2 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Rukwa ambapo amepokea changamoto kutoka kwa wanawake wengi  kuhusu utoaji mdogo wa mikopo na wengine kutopata kabisa mikopo kutoka Halmashauri zao.
Ummy amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashuri zote nchini kutenga asimilia 4 kwa ajili ya wanawake na kutoa mikopo yenye tija itaakayoweza kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi na sio kurudi nyuma kiuchumi.
“Mikopo ya laki tatu haina tija toeni kikopo yenye tija itakayoendana na kauli mbiu ya kuelekea uchumi wa viwanda,”alisema  Mhe. Ummy
Mhe. Ummy ameongeza kuwa ili kufikia azma ya Tanzania ya Viwanda basi Halmashauri hazina budi kujiwekea mikakati ya kutoa mikopo mikubwa itakayo wawezesha wanawake na wananchi kwa ujumla kufikia dhana hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kalembo Mhe. Julieth Binjula ameiomba Serikali kuendelea kuwawezesha wanawake kwa kuwapa elimu ya jinsi ya kutumia fedha na kuendesha miradi mbalimbali itakayo wakwamua kiuchumi.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Khalfan Haule amesisitiza wadau kushirikiana na Serikali pale ambapo wanaweza kuwawezesha wanawake sehemu walipo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kutoa mchangokatika kuchangia kujiletea maendeleo jumuishi.
Siku ya Wanawake Duniani 2018 kilele chake ni siku ya tarehe 8 Machi, 2018 na  Kaulimbiu inayoongoza maadhimisho haya ni‘‘KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA: TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WA WANAWAKE VIJIJINI”. Dhamira ya Wizara nikuona kila mdau mmoja mmoja anaelewa madhumuni ya kaulimbiu na kuchukua hatua kuchangia utekelezaji wa ujumbe mahususi wa kuwajumuisha wanawake wa vijijini katika maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.
CHANZO: DEWJBLOG
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post