Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Elimu Tanzania Graceana Shirima amesema ni matumaini yao kuwa fedha hizo zitatumika kwa ufanisi mkubwa na makusudio waliyoyaweka na matokeo yake yaonekane kwani kiasi kilichotolewa ni kikubwa.
Wakati akikabidhi #fedha hizo katika hafla iliyofanyika kwenye ukubi wa shule hiyo, Bi. Graceana amesema lengo la ukarabati huo ni kuhakikisha kuwa shule inakuwa na mazingira mazuri kwa ajili ya kupata elimu iliyokusudiwa na kuongeza ufaulu kwani miundombinu ya maabara, maktaba na madarasa vyote vitakarabatiwa na kuwa na mwonekano mzuri kwa mwanafunzi kusoma.
“Tuna imani uongozi wa Halmashauri ya Mji na Bodi ya #Shule hawatatuangusha katika usimamizi na watatumia fedha hizi kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha taratibu zote za manunuzi zinazingatiwa na hatutasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayekwenda kinyume na taratibu za manunuzi sababu mradi huu force akaunti ambayo inatumia jamii zaidi” Alisema Bi Graceana
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Hamza Mafita ametoa shukrani kwa serikali kwa kuwaletea fedha zote za mradi kwani fedha hizo zitabakia kwa wananchi wa Kondoa kwani mafundi watanunua vifaa vyote Kondoa na mafundi ni wenyeji wa Kondoa na kuwataka mafundi kumaliza mradi huo kwa wakati na haoni sababu ya kuchelewa ikiwa fedha zote zipo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji #Kondoa Khalifa Kondo akipokea mradi huo alisema kuwa anashukuru kupata mradi huo sababu ingekuwa ni jukumu la Halmashauri kukarabati kwa kutumia mapato ya ndani na kuahidi kuzisimamia fedha hizo kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri na Bodi ya shule ili kuhakikisha lengo la mradi linakamilika.
Mamlaka ya #Elimu Tanzania imetoa kiasi zaidi ya bilioni kumi kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe Tanzania ikiwemo Shule ya Wasichana Kondoa ambapo imepewa shilingi bilioni moja kwa ajili ya ukarabati wa #majengo ya shule hiyo
No comments:
Post a Comment