ODINGA ASEMA ATAANZA KUFANYA KAZI RASMI KAMA RAIS WA WATU

Image result for raila odinga

Kiongozi mkuu wa Muungano wa NASA Raila Odinga amesema ataanza kufanya kazi kama rais wa watu na hatishwi na lolote. #Odinga amesema hayo katika hafla mazishi ya bzbz yake na mkurungenzi wa mawasiliano wa chama cha ODM Philip Etale yaliyofanyika katika eneo la Embusakami jimbo la Vihiga. Aidha Raila ameishutumu serikali ya Jubilee kwa kuingilia majukumu ya idara ya Mahakama na kupuuza maagizo ya mahakama.
Vile vile amelaumu serikali ya jubilee kwa kutumia idara ya polisi kuwahangaisha viongozi wa upinzani
#Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Amos Wako ambaye alitetea Raila Odinga dhidi ya kushtakiwa na kosa la uhaini kufutia kuapishwa kwake.
Hata hivyo, kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi hakuhudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika ngome yake ya kisiasa, suala ambalo liliwatia hofu wafuasi wengi wa muungano wa NASA huku wengi wao wakihofia ushirikiano miongoni mwa vigogo wa muungano huo.
Ikumbukwe kwamba Muasilia Mudavadi, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula vile vile hawakudhuria hafla ya kuapishwa kwa Raila Odinga, jambo ambalo lilipokelewa na hisia tofauti miongoni mwa wafausi wa #NASA huku wengine wakidai kwamba, vinara hao watatu ni walisaliti wa bwana Odinga. Hata hivyo, Raila aliwahakikishia wafuasi wa NASA kwamba muungano huo uko imara na utaendelea kushirikiana kwa vyovyote vile.
Katika siku za hivi karibuni, kwenye mahojiano na shirika la utangazi la kimataifa la BBC Odinga alidokeza kwamba anataka uchaguzi uandaliwe upya kufikia mwezi wa Agosti mwakani, ikiwa ni siku chache tu baada ya serikali ya Jubilee kutangaza msako mkali dhidi ya viongozi wa upinzani, hasa wale waliohusika katika kuandaa hafla ya kuapishwa kwake Raila.
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post