Tanzania yaridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 kwa wasafirishaji wa mizigo

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. CharleS Mwijage(Mb) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania imeridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 (USD40) inayotozwa kwa kila stika kwenye magari yanayosafirisha mizigo kwenda nje ya nchi. Hatua hii imefikiwa kwenye Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha

Akizungumza katika Mkutano huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema Tanzania imefikia hatua hii ikiwa ni moja ya jitihada za kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini na Jumuiya kwa ujumla.

Tozo hii imekuwa ikitozwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa malori yanoyosafirisha mizigo kwenda sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya nchi. B

aada ya tathimini Serikali imebaini kuwa tozo hii inasababisha usumbufu na kuongeza gharama kwa wasafirishaji wa mizigo. Hata hivyo hatua hii inaendelea kuifanya Tanzania kuwa mtekelezaji mzuri wa makubaliano na itifaki mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huu uliofanyika kwa kipindi cha siku tatu tarehe 7 hadi 9 Februari 2018, pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili na kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru (NTBs) ambavyo vimekuwepo kwa muda mrefu katika Jumuiya. Mkutano huu umefikia tamati leo katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.

Taratibu za kuanza kufuta tozo hii zinaanza kutekelezwa mara moja.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano yaSerikali,
Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki,
9 Februari 2018


Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post