Waziri wa Nchi, Ofisi ya rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za mitaa, Tamisemi, Seleman Jafo, amegoma kuzindua mradi wa
maji katika kijiji cha Itiso wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kutokana na
baadhi ya wananchi kuharibu kwa makusudi miundombinu hiyo
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Waziri Jafo, amesema
awali mkandarasi wa mradi huo alisuasua na halmashauri ya chamwino na kuamua
kumbadilisha mhandisi wa maji ili kuweza kukamilika kwa haraka na kiwango bora.
Amesema wananchi wa kijiji hicho wamekuwa hawana Ushirikiano na
viongozi wao na wale wa mradi hadi kusababisha kuharibu miundombinu ya maji, na
kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya chamwino kusimamia na wale watakaoharibu
miundombinu washughulikiwe.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Athumani
Masasi, amesema serikali ya awamu ya tano imetoa kiasi kikubwa kwa ajili ya
mradi wa maji lakini wananchi wamekuwa mstari wa mbele kuharibu miundombinu
hiyo.
No comments:
Post a Comment