KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema ni marufuku
kwa mwanachi yoyote kushiriki kwenye maandamano kwani hawapo tayari kuona watu
wakiandamana na kusababisa uvunjifu wa amani iliyopo.
Mambosasa
ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mambo mbalimbali
na ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kutojihusisha na maandamano.
Amefafanua
kwenye mitandao ya kijamii kuna baadhi ya watu wanaitumia vibaya na sasa
wameanza kuhamasisha maandamano kwa kupanga tarehe ambayo itakuwa Aprili 26
mwaka huu.
“Kwenye
mitandao ya kijamii tumeona watu wanahamasisha maandamano.Tunawaambia Polisi
hatutakaa kimya na wale ambao wataandamana kitakachotokea wasitulaumu.
“Polisi
tumejipanga kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na wanafurahia
hali ya ulitulivu iliyopo.Wale ambao wanataka kufanya maandano wahesabu hawana
bahati na ndio maana tunaomba wananchi wasishiriki kwenye maandamano ambayo
yameanza kuhamasishwa kupitia mitandao ya kijamii,”amesema Mambosasa.
Amefafanua
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linataka kuona wananchi
wakiendelea na shughuli zao za kimaendeleo na wachache wenye kutaka kuvuruga
amani iliyopo haitawavumilia.
CHANZO: FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment