Naibu Waziri wa Maji
na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameagiza wakandarasi wote wanaotekeleza vizuri
miradi ya maji nchini walipwe fedha zao kwa wakati, bila kucheleweshwa
wanapoleta hati zao za madai, wakati alipokua akikagua utekelezaji wa miradi ya
maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Aweso
alisema pamoja na madai yao kulipwa kwa wakati, pia wakandarasi hao wapewe
miradi mingine zaidi kama mfano kwa wakandarasi wengine, kwani nia ya Serikali
ni miradi iishe kwa wakati na kufanya kazi na wakandarasi wenye uzalendo.
Katika ziara hiyo
Naibu Waziri Aweso alitembelea miradi ya maji ya Hondogo, Kibamba, King’azi A
na mradi wa kuchakata majitaka wa DEWAT uliopo Mburahati, unaofadhiliwa na
Taasisi ya Kijerumani ya BORDA akiambatana na wataalam kutoka DAWASA na
DAWASCO.
Manispaa ya Ubungo
imetengewa zaidi milioni 653 kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi ya maji, asilimia 60 ya fedha hizo zikiwa ni mapato yake ya ndani.
No comments:
Post a Comment