WANASHERIA
zaidi ya 100 wameanza kupitia na kuchambua malalamiko mbalimbali ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa
lengo la kuhakikisha
yanapatiwa majibu.
Hatua
hiyo inatokana na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufika kwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda na kisha kutoa malalamiko
kuhusu mambo
mbalimbali.
Kutokana
na malalamiko hayo Makonda aliaahidi kuyashughulikia na sasa timu hiyo ya wataalamu wa masuala ya sheria wameanza jukumu la
kupitia malalamiko ya wananchi hao na kisha kutafuta ufumbuzi wake wa kisheria.
Akizungumza
leo, Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Fabiola Mwingira
amesema wanasheria hao wameanza kufanya uchambuzi wa malalamiko hayo na baada
ya hapo wataanza
kuyasikiliza kwa
kukutanisha pande zote mbili kwa maana ya mtoa malalamiko na anayelalamikiwa.
“Wanasheria
hao wameanza kufanya uchambuzi wa malalamiko ya wananchi kuanzia leo hadi Machi 9 mwaka huu na lengo
kila mwananchi
aliyepeleka malalamiko yake basi yapate ufumbuzi.
“Malalamiko
wanayoyashughulikia ni yale ambayo hayako mahakamani na yaliyo mahakamani basi yatabaki huko huko yapatiwe
ufumbuzi na tayari wamewaandikia barua wahusika,’amesema Mwingira.
Amefafanua
baada ya wanashera hao kumaliza kusikiliza malalamiko hayo, watatoa ushauri wa kisheria ambao utamuwezesha
sasa Mkuu wa Mkoa
kutoa uamuzi.
Pia
amesema utoaji majibu ya kero za wananchi hao awamu ya pili ,majina yatabandika
kwenye geti la ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,hivyo wananchi watatangaziwa siku na saa.
No comments:
Post a Comment