TEMEKE : DC ASHUSHA NEEMA KWENYE SEKTA YA AFYA, ULINZI NA ELIMU

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva ameeleza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama tawala CCM ambapo ametaja miradi inayojengwa kwenye sekta ya elimu, afya pamoja na ulinzi na usalama.
Wakati akitoa ripoti ya utekelezaji wa ilani hiyo kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM- UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, Lyaniva amesema ofisi yake inahakikisha inaimarisha hali ya ulinzi na usalama, ambapo kwa sasa inajenga vituo vikubwa viwili vya Polisi maeneo ya Chamanzi na Toangoma, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Kwa upande wa sekta ya afya, Lyaniva amesema kuna vituo viwili vya afya vya kisasa vinajengwa katika Kata ya Yombo na Majimatitu ambapo vitakuwa na wodi ya kinamama na vyumba vya operesheni, ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali za Temeke na Zakhiem.
Kuhusu sekta ya elimu, Lyaniva amesema wanaongeza madarasa kwenye baadhi ya shule za msingi ili kupunguza msongamano wa wanafunzi hali iliyosababisha na utekelezwaji wa sera ya elimu bila malipo ambapo wazazi wengi wamekuwa na mwamko wa kuwaandikisha watoto wao shule.
“Suala la elimu bila malipo wananchi wameliitikia vizuri sana sababu wameweza kujitokeza wengi kuwaandikisha watoto wao shule, shule ya Majimatitu imeongoza kwa uandikishaji, ikifuati mbande. Palipokuwa na elimu ya malipo watu walikuwa majumbani wengi sana, nina uhakika hatutakuwa na watoto nyumbani, sasa hivi uhalifu umepungua hatuna kundi la kumi nje kumi ndani kwa kuwa watoto wanaenda shule,” amesema.
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post