Rais Mstaafu Kikwete amesema umefika
wakati busara kutumika kupunguza changamoto za wakimbizi miongoni mwa nchi za
Afrika ikiwa siku chache zimepita tangu Tanzania itangaze msimamo wa
kutoendelea kuwapa nafasi ya ajira, ukazi wa kudumu, umiliki ardhi.
Akizungumza kwenye mkutano wa jopo la viongozi mbalimbali
duniani lililoundwa kuangalia mfumo wa kuhudumia wakimbizi na jinsi ya kumaliza
migogoro iliyopo katika nchi mbalimbali, jijini Dare s Salaam, Dk. Kikwete
amesema, jopo hilo pamoja na mambo mengine limekutana kupokea taarifa ya changamoto
na kujua jinsi gani nchi zenye uwezo mdogo zinaweza kusaidiwa na Jumuiya ya
Kimataifa.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Dk. Augustine Mahiga, amesisitiza msimamo wa Tanzania wa kutoendelea
kuwapa nafasi ya ajira, umiliki wa ardhi na ukazi wa kudumu wakimbizi kwa
kutumia mkopo wa Benki ya Duniani bila kuzingatia mikataba ya Kimataifa iliyopo
na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa ingilie kati suala hilo.
Aidha amesema, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya
kujiridhisha na kuona ukiukwaji wa mikataba ya kimataifa ya kusaidia wakimbizi
inakiukwa pamoja na msaada wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi, UNHCR bado
halikidhi mahitaji yaliyopo na kukanusha si kweli kwamba Tanzania haitaki
kusaidia wakimbizi.
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment