Picha kwa hisani ya mtandao(haihusiani na tukio) |
Vifaranga 5,000 na trei za mayai 416
kutoka nchi jirani ya Kenya ambavyo vilikamatwa vikiingizwa nchini kinyume na
sheria vimeteketezwa moto kwa kuzingatia haki za wanyama.
Vifaranga hao walikamatwa katika eneo la mpakani mwa Kenya na
Tanzania Namanga ambapo baada ya kukamatwa vifaranga wa kuku wa mayai 5000
wenye thamani ya Tsh 11,500,000 na Trei 416 zenye mayai, yenye thamani ya
3,120,000/ kwa pamoja viliteketezwa kwa moto kwa kuzingatia haki za wanyama
(Animal welfare) ambapo kabla ya kuteketezwa mifugo hiyo ililazwa kwa kutumia
dawa aina ya Farmaldehyde na kuhakikisha wamekufa kabla ya kuchomwa.
Mayai hayo pamoja na vifaranga vimekamatwa vikiingizwa nchini
kinyume na sheria, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la chakula (FAO) ya
mwezi Desemba ilitoa taadhari kuwa nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani Kenya
na Uganda na nchi nyingine za Afrika ziko hatarini kuambukizwa mafua makali ya
ndege
No comments:
Post a Comment