Naibu waziri wa maji Mhe Jumaa Aweso
ameagiza mhandisi wa manispaa ya Temeke Damas Shirima kukamatwa na kuhojiwa na
polisi kwa kosa la kutoa maelezo yasiyo ridhisha juu ya utekelezaji wa mradi wa
maji wa mwasongo uliopo Kigamboni Dar es salaam.
Akizungumza katika majumuisho ya siku yake ya pili ya ziara yake
jijini Dar es salaam Mhe Aweso amesema kuwa serikali haiwezi kunyamaza kimya
pale inapooneka miradi ya maji inahujumiwa waziwazi na kwamba watahakikisha
wale wote ambao wanagundulika kuhujumu miradi ya maji hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
Awali mbunge wa jimbo la Kigamboni ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Afya Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa jimbo lake bado linachangamoto ya
upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo ambapo amehaidi kulisimamia suala hilo
ili wananchi waondokane na kero hiyo.
chanzo: eatv
No comments:
Post a Comment