Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za Iparamasa pamoja Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu. |
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa. |
Meza kuu ikiongozwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani. |
Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu. |
Waziri
wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi
shirika la White City Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea
awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.

Hayo
aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na
kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Wilayani Chato ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa
kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.

Mmoja
kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea
kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara
zao.
kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara
zao.
Aidha
kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la
Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo kwa Mkandarasi
kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia
siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.
“Nimesikia
kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia
nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe
amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa
nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.
Mradi
wa usambazaji wa umeme vijijini Mkoani Geita,unatekelezwa na mkandarasi
wa Shirika la White City International ambapo unatarajia kufanyika ndani
ya miezi 16 kwenye jumla vijiji 220 vilivyopo mkoani
humo na jumla ya fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo
ni Sh Bilioni 78.56.
No comments:
Post a Comment