Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali moja ya mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda
SERIKALI
yaendelea kuongeza vituo vya Afya nchini ikiwa ni moja ya jitihada za Serikali
za kuboresha Huduma za afya nchini jambo litakalo saidia kupunguza msongamano
wa wagonjwa katika Hospitali za Wilaya na Mkoa kwa kuwa huduma zote zitakuwa
zimeishia kwenye ngazi ya Kata.
Hayo
yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa wakati wa ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali
ya Amana, mapema leo jijini Dar es salaam.
“Kumekuwa
na ongezeko kubwa la vituo vya Afya nchini kutoka vituo vya Afya 6321 kwa mwaka
2010 hadi vituo vya Afya 7680 kwa mwaka 2016, na kazi ya nyongeza inaendelea,
kwaiyo tunaamini vituo hivi vitaweza kupunguza msongamano katika
hospitali za Wilaya, pamoja na Hospitali za Mkoa”, alisema Mhe. Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa.
Mhe.
Waziri Mkuu alisema kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ametenga kiasi cha Zaidi ya Bilioni 100 ikiwa ni fedha za
kuboresha Vituo vya Afya nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi
katika maeneo yote nchini.
“Tumeanza
kuboresha Vituo vya Afya kwa kujenga Wodi yakinamama wanaojifungua, thieta,
wodi za magonjwa yakawaida, maabara, tunaongeza na nyumba za watumishi, ili
kila kituo cha Afya kiwe na miundombinu hiyo ili utoaji huduma uwe rahisi”
alisema Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe.
Waziri Mkuu aliendele kusema kwamba Serikali imetumia Zaidi ya Bilioni 161
katika kuendelea kuboresha Huduma za Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa Maisha
ya mama na mtoto jambo ambalo ni moja kati ya changamoto kubwa nchini.
Aidha
Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba Serikali imeendelea kuboresha Huduma za Afya
kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 129 kwaajili ya vifaa vya kuwezesha
kundesha shughuli za upasuaji katika kila kituo cha Afya ambacho kinaboreshwa.
Wakati
akitoa taarifa ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda alisema
kwamba wakina mama 126,164 walipata nafasi ya kujifungua katika vituo vya Afya,
huku wakinamama 202 ambao ni sawa na Asilimia 0.5 walilazimika kujifungua kwa
wakunga, na Asilimia 1.5 zaidi ya akinamama 1976 walijifungua njiani wakielekea
kupata huduma, idadi inayoonekana kuwa kubwa sana katika Mkoa wa Dar Es salaam.
Idadi
ya 2016 inaonesha Zaidi ya akina mama 85 walikuwa wanapoteza Maisha kati ya
kina mama 100,000 waliokuwa wanajifungua lakini kwa sasa tangu maboresho
yafanyike ni akina mama 57 kati ya akina mama 100,000 wanaojifungua ndio
hupoteza Maisha, huku mikakati thabiti yakupunguza vifo hivyo ikiendelea
kuwekwa.
Mhe.
Makonda aliendelea kusema kwamba zaidi ya watoto ambao wanafanikiwa kuwa hai na
kuwa salamakatika kujifungua ni Zaidi ya watoto 126,712, na watoto 131 huzaliwa
wakiwa tayari wameshakufa, idadi hii ikilinganishwa .
Pia
Mhe. Makonda alimshukuru AMSONS GROUP ambayo imetoa mchango mkubwa katika
ujenzi wa Jengo hilo la Mama na Mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana huku
akiwataka Wadau wengine kuiga mfano huo katika dhana ya kusukuma gurudumu la
maendeleo katika jamii zetu.
Nae
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani
imeongeza Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 mpaka sasa ni Bilioni 270 likiwa ni
ongezeko la Zaidi ya mara 9, huku Wastani wa upatikanaji wa dawa ukiwa Zaidi ya
asilimia 80.
“Serikali
wakati inaingia madarakani Bajeti ya dawa ilikuwa ni Bilioni 30, mwaka
unaofuata ikafikia Bilioni 200, na hivi tunavyoongea Bajeti ya Dawa ni Bilioni
270, likiwa ni ongezeko la mara 9, kama msaidizi wako nasimama kifua mbele
No comments:
Post a Comment