MTWARA: SERIKALI IMESEMA HAIJARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA BARABARA YA MTWARA MNIVATA

Image may contain: 4 people, people smiling, people standing, beard and outdoor
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mh MAKAME MBALAWA amepozungumza na Wananchi wa Kata ya Naliendele Jana Tarehe 4/3/2018 na kumtaka Mkandarasi anaejenga Barabara hiyo kwa kiwango cha Lami kuharakisha ujenzi huo.

Waziri MBALAWA mesema"Haturidhishwi na kasi ya Ujenzi wa barabara hii yenye Urefu wa Km 50 Kutoka Mtwara hadi Kijiji cha Mnivata kwa Thamani ya Tsh Bilioni 89.59 na ndio maana tunatembelea mara kwa mara kumsukuma Mkandarasi huyu afanye kwa kasi tunayoitaka"

Akijibu maswali ya baadhi ya Wananchi waliouliza kuhusu Swala la wenyeji kukosa Ajira ndogondogo na kupewa watu wa Mikoa mingine pamoja na kukosa miundombinu itakayosaidia maji yasituwame katika eneo moja, Waziri huyo amesema atayafanyia kazi kama Serikali.
Image may contain: one or more people, people standing, sky, tree, outdoor and nature 
Waziri Mbalawa aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara MH EVOD MMANDA ambae nae alipata nafasi ya kuzungumza na Wananchi hao na kuwasihi waendelee kushirikiana na Mkandarasi huyo ili barabara hiyo iweze kukamilika kwa haraka.

Karim Faida-JAMII FM.


Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post