BERLIN: TANZANIA YAJITANGAZA KITALII UGHAIBUNI


Katibu Mkuu wa Wizara ya maliasili na italii Mhe, Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi ameongoza msafara wa Tanzania unaoshiriki katika maonesho ya kimataifa ya Utalii ya ITB 2018 yanayoendelea kufanyika Jijini Berlin nchini Ujerumani.
Lengo la Maonesho hayo ni kutangaza fursa za utalii zilizopo nchini hapa Tanzania katika masoko mbalimbali ya utalii barani Ulaya na duniani kote.
Maonesho hayo yalianza tarehe 7 mwezi huu na yanatarajiwa kufikia tamati hapo keshokutwa tarehe 11 Machi, 2018. Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo umehusisha Sekta ya Umma na Sekta mbalimbali Binafsi.
Ambapo washiriki kutoka sekta ya umma ni pamoja na idara ya utalii kutoka wizara ya maliasili na utalii,bodi ya utalii Tanzania,shirika la hifadhi za taifa,mamlaka ya hifadhi Ngorongoro na mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania.
Kwa upande mwingine sekta binafsi jumla ya kampuni zipatazo 60 zimeshiriki maonyesho hayo ikiwemo kampuni moja inayoshughulika na uratibu wa matukio (Events and Exhibitions management),kampuni tatu zinazoshughulika na usafiri wa anga,kampuni ishirini na saba(27) zinazoshughulika na huduma za malazi yaani hoteli,loji na kambi za utalii na kampuni ishirini na tisa(29) za Wakala wa biashara ya kusafirisha watalii.
Pamoja na shughuli za maonyesho hayo katibu mkuu Milanzi amefanya pia mikutano kadhaa na wadau wa utalii na washirika wa maendeleo waliopo nchini Ujerumani.
Sekta ya utalii inachangia wastani wa asilimia ishirini na tano(25%) ya fedha zote za kigeni zinazoingia nchini kwetu Tanzania huku ikichangia asilimia kumi na saba na nusu(17.5) ya pato la Taifa.

CHANZO: DARMPYA
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post