DAR ES SALAAM: KUBENEA "DC HAPI KADANGANYA UMMA, NIMEONDOKA MWENYEWE OFISINI"

Mbunge wa jimbo la Ubungo, Mhe. Said Kubenea, amepinga vikali taarifa inayodaiwa kutolewa na mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mhe. Ally Hapi, ikiuhabarisha umma kuwa wabunge Halima Mdee (Kawe) na Said Kubenea (Ubungo), wamefukuzwa kwenye ofisi walizokuwa wakizitumia kwenye jengo la wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza na wanahabari asubuhi ya leo Jumamosi Machi 10, 2018, Mhe. Kubenea amesema mkuu wa wilaya hiyo ameamua kutumia jina lake (Kubenea) ili kujipatia umaarufu maana taarifa ya mkuu wa wilaya imekuja ikiwa tayari yeye ameshahama kwenye ofisi hizo.
Katika hatua nyingine Mhe. Kubenea amewataka vijana walioaminiwa na Mhe. Rais, na kupewa madaraka, wasilewe madaraka hayo na kujiona wao miungu watu, huku akisema vyeo walivyonavyo kwasasa ni vya kupita tuu maana walikuwepo waliokuwa navyo kabla yao, hivyo wawatumikie wananchi kwa kuzingatia utawala wa sheria bila kuwabagua wapinzani.
Mhe. Kubenea amehitimisha mkutano wake na wanahabari kwa kumsihi Mhe. Rais Magufuli atazame yale yanayofanyika kwa majirani zetu Kenya, ambapo Rais Uhuru Kenyatta alikutana na mpinzani wake Raila Odinga, na kufanya mazungumzo naye kwa maslahi ya wakenya wote, hivyo kumuomba Rais Magufuli asiwachukulie wapinzani kama maadui, bali watu wanaompa changamoto ili kulisaidia taifa, na hivyo hanabudi kushirikiana nao.

CHANZO: DARMPYA
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post