Wakazi wa kijiji cha Maguruwe wilayani #Mvomero Mkoani
Morogoro wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwathamini
na kuweza kufika kwenye kijiji hicho mteule wa Rais ambaye ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, #TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo, kwa kuwa hakuna kiongozi wa ngazi ya Uwaziri ambaye amewahi kufika
kwenye eneo hilo.
Kutokana na Waziri Jafo kuwa Waziri wa kwanza kufika
kwenye kijiji hicho wazee wa kimila wa kijiji hicho walimsimika na
kumpa heshima maalum ya waluguru.
Wakizungumza huku wakiwa wamejawa na furaha, Wananchi
hao wamesema kijiji chao ambacho kipo juu kabisa ya safu za
milima ya Ulugulu hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya uwaziri aliyewahi kufika maeneo hayo kwa kuwa barabara
zake hazipitiki kirahisi.
Wamesema wamefurahishwa na kiongozi huyo kwa kuweza kuwafikia
walipo hali ambayo imewafanya kujisikia furaha.
Katika ziara hiyo ya kikazi, Waziri Jafo amefanikiwa
kuzindua vyumba vitatu vya madarasa vilivyojengwa na Taasisi ya CDTF.
Hata hivyo, kutokana na changamoto kubwa
ya barabara katika eneo hilo, Waziri Jafo alimuagiza meneja wa TARURA wilaya ya Mvomero kufanya
tathmini ya barabara hiyo ili serikali ione jinsi ya kuifanyia kazi hapo baadae ili wananchi hao waweze kuondokana na
adha hiyo.
No comments:
Post a Comment