Katika hali iliyowashtua wengi, jeshi la polisi wilayani Kondoa
mkoani Dodoma lililazimika kupiga risasi takribani sita ilikukabiliana na
watu walikuwa kwenye harakati za kuuziana vipande tisa vya meno ya tembo
katika wilaya hiyo.
Hayo yamebainishwa Jana Ijumaa Februari
23, 2018 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
Gilles Muroto, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Kamanda Muroto alisema jeshi hilo
linawashikilia watu wanne waliokamatwa wakiwa kwenye harakati ya kuuziana
vipande tisa vya meno ya tembo yenye uzito wa kilo 2.450 na thamani ya shilingi
milioni 67.5, baada ya kukutwa wakiwa karibu na maeneo ya benki ya NMB wilayani
Kondoa.
Kamanda Muruto amesema mara baada ya
watuhumiwa kuona wamezingirwa na polisi walijaribu kutoroka kwa kuwatishia
askari kwa visu, lakini askari walilazimika kufyatua risasi sita hewani na
kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote.
Aidha kamanda Muroto aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na: Juma Gindae (50), mkulima na mkazi wa
Kwamatoro wilaya ya Chemba mkoani Dodoma na Patrick Mwaluko (49), mkulima mkazi
wa Kidoka wilaya ya Chemba, Daudi Masinga (22), dereva wa bodaboda na
mkazi wa Kidoka, na Khalifa Saluti (21), dereva bodaboda ambaye pia ni
mkazi wa Chemba.
No comments:
Post a Comment