Mbunge wa Kigoma mjini ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT
Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe, mchana wa leo Jumamosi Februari 24, 2018
amezungumza na wanahabari akiwa moja kwa moja kwenye mtandao wa kijamii
Facebook, ambapo amezungumzia masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.
Katika mkutano huo Zitto
ameambatana na viongozi wengine akiwemo mwenyekiti wa chama hicho mkoani
Arusha,na Mwenyekiti, Kamati ya Sera na Utafiti wa chama hicho
ndugu Emmanuel Lazarus Mvula.
Mhe. Zitto amezungumzia
kuhusu uminywaji wa demokrasia nchini, matukio ya mauaji ya raia na wanasiasa,
pamoja na kukosekana kwa uwiano wa huduma za kijamii na rasilimali kati ya
maeneo ya mijini na vijijini.
Akizungumzia suala la
demokrasia nchini, Mhe. Zitto amesema kumekuwa na tishio kubwa la uminywaji wa
demokrasia nchini ikiwa ni pamoja na uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano
yake, jambo ambalo ni kinyume kabisa na katiba ya nchi.
“Nchi yetu ni ya demokrasia ya vyama
vingi, ni wajibu wa kila mtanzania kulinda demokrasia hii, Kwakuwa kuna dalili
zote za kurudishwa kwenye mfumo wa chama kimoja, ni wajibu wa watanzania kujitokeza
kupinga mambo haya” amesema
Zitto
Akizungumzia matukio ya mauji
ambayo yamekuwa ya kiendelea hapa nchini dhidi ya wanasiasa, na wananchi wa
kawaida, Mhe. Zitto amesema chama chake kina laani vikali matukio hayo, huku
akiitaka serikali kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika.
“chama chetu kinalaani vitendo vya
mauaji nchini kwa nguvu zote” amesema Zitto.
Akiongelea kuhusu uwiano wa
upatikanaji wa huduma za kijamii nchini, Zitto ameseam hakuna uwiano wa
rasilimali kati ya mjini na vijijini, akitolea mfano wilayani Kibaha kuwa shule
za maeneo ya mjini zina walimu wa kutosha huku zile zilizopo maeneo ya vijijini
zikikosa walimu wa kutosha.
Zitto amehitimisha mkutano
huo kwa kupendekeza kuundwa tume huru itakayochunguza masuala ya mauji ya
kisiasa nchini na yale ya wananchi wa kawaida, pia kuchunguza vitisho vya
mauaji vinavyotolewa dhidi ya wanasiasa.
Zitto pia amependekeza
kuhitishwa kwa mkutano wa kitaifa wa kujadiliana masuala ya kisiasa nchini
ikiwa ni pamoja na mstakabali wa vyama vya siasa nchini, na kama serikali
haihitaji mfumo wa vyama vingi basi walete pendekezo la kuwa na chama kimoja.
No comments:
Post a Comment