DAR ES SALAAM: DIWANI KATA YA KIBONDE MAJI AISHUKURU OFISI YA MKUU WA MKOA

Diwani wa kata ya Kibonde Maji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati yaHuduma za Jamii katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mhe.  Abdallah Mtinika, ameishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwapatia reflector 300 vijana wa bodaboda katika kata yake.
Mhe. Mtinika ameyasema hayo leo  Jumamosi Februari 24, 2018 alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa utambulisho wa kikundi cha waendesha bodaboda kata ya Mbagala Kibonde Maji jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mtinika ameyasema hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya Temeke, ndugu Felix Lyaniva, ambapo amesema wao kama viongozi walichokifanya ni kuwaunganisha vijana kufanya kazi kwa pamoja na kushiriki katika kulinda usalama wa eneo hilo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mtinika amelipongeza jeshi la polisi katika maeneo hayo kwa kufanya kazi zake kwa weledi, huku akiwalaumu baadhi ya mgambo ambao wamekuwa wakikamata raia kinyume na taratibu.
Aidha Mhe. Mtinika amesema wataendelea kushirikiana na taasisi na mashirika mbalimbali katika kusimamia ulinzi na usalama wa eneo hilo, huku akisema kuna vijana wa kujitolea ambao watakuwepo kwenye ofisi za kata kwaajili ya kutoa msaada wa huduma za kisheria
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post