Rais Magufuli amezuia kuondolewa kaya zaidi 1,900 zinazoishi
katika nyumba zilizopo karibu na uwanja wa ndege wa Mwanza hadi serikali
itakapofanyika tathimini yakufidia wananchi hao ambao ni wapiga kura wake.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo
Februari 24, 2018 baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa
Uwanja huo ambao walimweleza Kuwa uwepo wa Kaya hizo unakwamisha Ujenzi wa
uwanja Huo.
“Hawa watu ndiyo walionipa kura, pamoja
na hivyo msiwaondoe hadi pale mtakapokamilisha kuwalipa madai yao,” amesema
Rais Magufuli.
Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli
aliagiza kusitishwa kwa ubomoaji wa nyumba za wananchi zaidi ya 2,000
wanaodaiwa kuvamia eneo la uwanja huo, kituo cha polisi na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ).
Siku hiyo wakati akizungumza na wananchi
wakati wa uzinduzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu eneo la Furahisha
jijini Mwanza, Rais Magufuli aliagiza ubomoaji huo usitishwe hadi atakapotolea
uamuzi suala hilo.
Leo mjini Mwanza, Meneja wa uwanja huo,
Ester Mandale alimweleza Rais Magufuli kuwa wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa jengo la wasafiri, Uwanja kukosa uzio pamoja
na ndege kuzuiwa kubeba samaki.
Amesema baada ya ndege kuzuiwa
kusafirisha samaki kwenda nchi za nje, wanalazimika kusafirisha kwa kutumia
magari wakati wenzao wa Kenya wanatumia ndege, hivyo kuikosesha Serikali
mapato.
Akizungumzia changamoto hiyo, Rais
Magufuli amemwagiza meneja huyo kufanya tathmini inayohitajika Katika Ujenzi wa
Jengo la Usafiri Pamoja na Uzio kisha Aiwasilishe Serikalini Kwa ajili Ya
kuanza ujenzi Huo.
Rais Ameondoka jijini Mwanza na
anaelekea Chato kwa ajili ya mapumziko.
No comments:
Post a Comment