WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kila kiwanda kilichopo nchini kihakikishe
kinatumia alama za utambuzi za GS1 Tanzania simbomilia (barcodes).
Ametoa
agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 22, 2018) wakati akifungua Mkutano wa Sita
wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes). Hadi sasa GS1 ina
wanachama 2000.
“Natoa
wito kwa wenye viwanda kutumia GS1 Tanzania kutangaza na kuuza bidhaa zenye
ubora katika maduka ya kimataifa, ambapo pia bidhaa zao zitachangia katika
ulipaji wa kodi kwa usahihi”.
Amesema
matumizi ya alama hiyo, iwe ndio chanzo cha kulipeleka Taifa kwenye kampeni ya
kuhamasisha jamii kununua bidhaa zilizotengenezwa nchini. Hadi sasa
Waziri
Mkuu amesema kama kila bidhaa itakuwa na utambuzi wa Taifa kiambishi “620”,
wataweza kuwa na takwimu sahihi za wazalishaji ambao wanatambulika.
Pia
Waziri Mkuu amesema utambuzi wa bidhaa zinazozalishwa nchini ukifanyika kwa
kutumia GS1 kila duka litalipa kodi kwa kila bidhaa inayouzwa.
Hata
hivyo Waziri Mkuu amesema barcodes ni muhimu kwa sababu zinawawezesha
wajasiriamali kuuza bidhaa zao katika maduka rasmi ya nje na ndani ya Tanzania.
Amesema
miaka ya nyuma kabla ya kuanzishwa kwa GS1 Tanzania, wazalishaji wa bidhaa za
Tanzania walilazimika kwenda nje ya nchi yetu
kutafuta barcodes ili waweze kuuza bidhaa zao.
Waziri
Mkuu amesema hali hiyo iliifanya Tanzania kuwa wategemezi na kuchangia
kuzalisha ajira kwa ajili ya nchi nyingine kwa kununua barcodes zao.
“Tangu kuanzishwa kwa chombo chetu, tumejinasua kutoka katika utegemezi huo.
Pia
Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na mipango iliyowekwa na GS1 Tanzania ya
kuhakikisha kwamba mazao ya kilimo yanapatiwa barcodes na
kuwaelimisha wananchi kuhusu alama hizo.
Mkutano
huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi
Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara SMZ, Balozi Amina Salum
Ally, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof.
Elisante Ole Gabriel.
Wengine
ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Dkt. Gidion Mazara, Wakuu wa Taasisi na
Wadau wa GS1 kutoka Tanzania Bara na Visiwani (TBS, BRELA, TANTRADE, ZNCIAAL,
COSTECH na Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatuma Kange.
No comments:
Post a Comment