Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso anatarajiwa kuongoza kikao baina ya uongozi wa Manispaa ya Ilala, DAWASA na DAWASCO ili kutafuta njia ya kupata fedha za kukamilisha mradi wa maji wa Kimbiji ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji kwenye maeneo kadhaa ya jiji ikiwemo wilaya hiyo.
Naibu Waziri aliyasema hayo Februari 12, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bonyokwa huko Kinyerezi Wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, baada ya kuambiwa kuwa awamu ya kwanza ya uchimbaji visima virefu 20, umekamilika na unakusudia kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji maji kwenye maeneo ambayo hayana mtandao wa maji.
“Mamlaka ya DAWASA ndio iliyopewa jukumu kusimamia awamu ya kwanza ya uchimbaji visima virefu vilivyo kwenye takriban mita 405 hadi 600 na viko 20 kilichobaki ni awamu ya uendelezaji wa visima (kuweka mtandao wa usambazaji maji ili maji yaweze kuwafikia wananchi wa jiji la Dar es Salaam likiwemo eneo hili.” alisema Aweso.
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, (DAWASA) Bi. Modester Mushi. Bi. Mushi alifafanua kuwa sababu ya kutenga mradi huo kwa awamu ni kutokana na gharama na upatikanaji wa fedha lakini akabainisha kuwa Mamlaka iko kwenye hatua nzuri kwa ajili ya kutekeleza awamu ya pili ambapo nyaraka ziko kwa Mwnaasheria Mkuu kwa ajili ya mapitio na kupitia Wizara wanategemea kuanza mradi huo kwa wakati katika mwaka wa fedha ujao, alisema.
Baada ya maelezo hayo ndipo Naibu Waziri ambaye alifuatana na Mbunge wa jimbo la Segerea Mhe. Bonna Kalua, aliagiza mkutano wa dharuara ufanyike Jumanne baina yake, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, DAWASA na DAWASCO ili kutafutia ufumbuzi mkwamo huo kwani wananchi wanataka maji na si vinginevyo.
Na Khalfan Said, K-Vis Blog
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso, (aliyesimama), akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa majumuisho ya ziara yake aliyoifanya kuangalia hali ya upatikanaji wa maji kwenye wilaya ya Ilala hususan jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam Februari 12, 2018.
Mhe. Aweso, akisikiliza kwa makini kero za wananchi kuhusu maji.
Baadhi ya wananchi wa jimbo la Segerea waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Bonyokwa Februari 12, 2018.
Mbunge wa jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, Mhe. Bonna Kaliua, akizunguzma na wananchi wa Bonyokwa kwenye mkutano huo.
Mbunge wa jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, Mhe. Bonna Kaliua, akizunguzma na wananchi wa Bonyokwa kwenye mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam, (DAWASA), Bi. Modester Mushi, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji jijini Dar es Salaam ikiwemo jimbo la Segerea.
Mwakilishi kutoka DAWASCO, akizungumza kwenye hadhara hiyo.
Meneja Uhusiano wa Jamii wa DAWASA, Bi. Neli Msuya, na wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia hotuba.
Mhe. Aweso na Mhe. Bonna Kalua, wakijadiliana jambo mwishoni mwa mkutano huo
No comments:
Post a Comment