Waandishi
wa habari nchini wametakiwa kutojihusisha na maswala ya kisiasa katika utendaji
wao wa kazi ili kuandika habari za ukweli na usahihi.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Waziri ya Habari, Tamaduni, sanaa Na Michezo JULIANA
SHONZA katika maadhimisho ya siku ya Redio duniani ambayo kitaifa yamefanyikia
Mjini DODOMA.
Naibu
waziri amesema waandishi wa habari wanajukumu la kufikisha habari kwa jamii ili
kulinda amani na upendo kwa kujali utu wa mtu.
Amesema
vyombo habari vina nafasi kubwa katika jamii na kama vikitumika kwa mrengo
sahihi itasaidia kuiunganisha jamii na serikali.
Maadhimisho
ya siku ya redio duniani kitaifa yamefanyika Mjini DODOMA ikiwa ni kwa mara ya pili kufanyika mkoani
humu. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ‘Redio na Michezo’ ambapo Naibu waziri
wa Habari, Utamadunii sanaa na Michezo Mh JULIANA SONZA amehudhuria kwa niaba
ya Waziri wa Wizara hiyo Dr. HARRISON MWAKYEMBE.
No comments:
Post a Comment