SERIKALI
ya Jamhuri ya Poland mapema mwezi April mwaka huu inatarajia kufungua upya
Ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini ambazo zilifungwa kwa muda, hatua
inalenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mataifa hayo.
Hayo
yamesemwa leo Ijumaa (Februari 23, 2018) Jijini Dar es Salaam na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipokuwa
Salamu za Rais wa Poland kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli.
Dkt.
Mwakyembe alisema hatua zote muhimu za ufunguzi wa Ubalozi huo, taratibu zote
muhimu kwa ajili ya ufunguzi Ofisi za Ubalozi huo tayari zimekamilika na
kuongeza kuwa kufunguliwa kwa ubalozi kutazidi kudumisha ushirikiano na urafiki
wa muda mrefu baina ya Tanzania na Poland pamoja na kuimarisha diplomasia ya
uchumi baina ya mataifa hayo.
“Serikali
ya Jamhuri ya Poland imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania, ambapo
matunda ya ushirikiano ni kwa Serikali yetu kupata wa mkopo wa masharti nafuu
uliofanikisha uanzishaji wa kiwanda kikubwa cha matrekta kibaha Mkoani Pwani”
alisema Dkt. Mwakyekmbe.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Krzysztof Szczerski
alisema ziara yake ya kuja nchini ni kuwasilisha salamu za Rais wa
Jamhuri ya Poland ambapo pamoja na mambo mengine Serikali ya nchi hiyo
imekusudia kuimarisha mahusiano yake ya kiuchumi na Tanzania.
Aliongeza
kuwaa katika kuendeleza jitihada zake za kuimarisha uhusiano wake na Tanzania,
Serikali ya Poland tayari inaendesha miradi mbalimbali ya uwekezaji nchini
ambapo Rais wa Poland ameahidi kuimarisha ushirikiano huo baina yake na Rais wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
“Niwewasilisha
salamu za Rais wa Jamhuri ya Poland ambapo pamoja na mambo mengine, amemualika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda nchini Poland kwa ajili ya ziara
maalum ya kiserikali” alisema Szczerski.
No comments:
Post a Comment