Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza
watalaamu wa elimu na viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuhakikisha wanaendeleza
Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania) unaotekelezwa na
Serikali kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la nchini Uingereza (DFID).
Makamu
wa Rais ametoa agizo hilo leo Mkoani Simiyu alipokuwa akiongea na viongozi na
watumishi wa Serikali wa Mkoa huo katika kikao cha majumuisho ya ziara
yake ya siku tano mkoani humo.
“Mpango
huu umekuwa na mafanikio makubwa kwa Mkoa wa Simiyu, kutokana na kuongezeka kwa
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya kitaifa ya darasa la Saba
ambapo Mkoa umetoka kushika nafasi za mwisho Kitaifa hadi kufikia nafasi ya 11
mwaka 2017.
Amesema
mafanikio ya mpango huo yamekuwa makubwa, huku akishukuru shirika la DFID kwa
mchango wao mkubwa ikiwa ni pamoja na kutoa kiasi cha fedha shilingi Bilioni
1.3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule.
Aidha,
Mhe. Samia ameutaka uongozi wa mkoa huo kuhakikisha Mpango huo unaendelezwa
hata baada ya wafadhili hao kumaliza muda wao ili kuhakikisha kiwango cha elimu
kinaendelea kuboreka kila mwaka.
Mhe.
Samia amemuhakikishia Kiongozi Mkuu DFID-Tanzania Bibi Elizabert Arthy
kuwa nchi ya Uingereza itaendelea kufanya kazi na Serikali katika kuboresha
elimu nchini.
Kwa
upande wake, Elizabeth Arthy amesema katika kuhakikisha wanapambana na hali ya
kuboresha elimu nchini tayari Mkoa wa Simiyu umepewa fedha kutoka DFID kiasi
cha shilingi Bilioni 1.3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameishukuru DFID kwa ufadhili wake kupitia
EQUIP-Tanzania ambapo ufaulu wa wanafunzi umeongezeka mkoani humo kutoka
asilimia 36 mwaka 2013 mpaka 68 mwaka 2017.
Katika
kipindi cha miaka Minne DFID imewekeza katika mpango wa kuinua ubora wa elimu
mkoani Simiyu kwa kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 9.
No comments:
Post a Comment