MASASI : KAMATI YAUNDWA KUFUATILIA MALIPO YA WAKULIMA WA KOROSHO

MASASI

MKuu wa Mkoa wa Mtwara MHE GELASIUS BYAKANWA ameunda kamati maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madai ya wakulima wa zao la korosho wilayani Masasi kufuatia wakulima wengi kulalamika kutolipwa malipo yao.
 Image may contain: 4 people, people sitting and indoor
Agizo hilo amelitoa Leo ( Feb 6 ) kwenye kikao kilichojumuisha viongozi wa Vyama vya ushirika ( AMCOS ) , wakulima na viongozi wa mabenki Lengo ikiwa ni kujua matatizo ya wakulima ili yatafutiwe ufumbuzi na hatimaye wakulima wapate haki yao.

BYAKANWA ameipa siku 14 kamati hiyo ambayo itaongozwa na MKuu wa wilaya ya MASASI kufanya uchunguzi huo na tarehe 22 mwezi huu kikao cha kuwasilisha taarifa ya uchunguzi huo kitafanyika.

Aidha ameagiza akaunti ya Katibu Wa Chama Cha Msingi Mmbaka isitoe fedha mpaka uchunguzi utakapo kamilika kutokana na katibu huyo kutolipa wakulima fedha tasilimu wakati utaratibu ulielekeza kila mkulima alipwe fedha zake kupitia akaunti na si vinginevyo.


UTEKELEZAJI WA AGIZO 

Kufuatia taarifa ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara  MHE. GELASIUS BYAKANWA  la kuunda kamati maalumu ya kufanya uchunguzi juu ya tatizo la baadhi ya wakulima wa zao la korosho Wilayani Masasi kutolipwa fedha zao, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi MHE. JUMA SATMAH amewata watendaji wa Kata wa Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano kwa kamati ya uchunguzi ili kuhakikisha takwimu sahihi za kila mkulima zinapatikana.

Image may contain: 4 people, people sitting


Hayo ameyasema jana Katika mkutano wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa za utekelezaji za Kata robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo ameeleza kuwa Watendaji wa Kata wana wajibu wa kufahamu idadi ya wakulima ambao hawajalipwa maana ni sehemu ya majukumu yao.

ikumbukwe kuwa wakulima wamekuwa na tatizo la kutopata malipo yao kutokana na kuhamia kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya bank ambapo wakulima wachache wamepata changamoto ya kutumia huduma za kibenki.


Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post