DODOMA
Mkufunzi kutoka Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni –UNESCO- BI ROSE HAJI
MWALIMU amewataka Waandishi wa habari nchini kuweka usawa wa kijinsia
wanapofanya kazi zao.
Waandishi wa Habari wakiendelea na mfunzo katika ukumbi wa TBA -DODOMA |
Yamesemwa hayo katika
mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa Wakala wa Majengo Mkoani
DODOMA ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kufanya kazi zao
kwa ufasaha na kwa uweledi.
Mkufunzi huyo amesema
iwapo Waandishi wa Habari watashindwa basi watakuwa hawajatenda haki katika
Jamii, kwani wengi wao wamekuwa wakifanya kazi bila kuzingatia usawa kijinsia
ambapo mara nyingi wanaume ndiyo wamekuwa wakipewa kipaumbele kuliko wanawake .
Mafunzo hayo
yanayaoendelea Mjini DODOMA yanatarajiwa kumalizika tarehe 12/2/2018 ambapo
yatahitimishwa na maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yatakayofanyika katika
ukumbi wa NASHEERA HOTEL mjini DODOMA
No comments:
Post a Comment