WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemkabidhi mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Stephen Kiruswa gari aina Tunland
Double cabin kwa ajili ya kuboresha huduma za chanjo na afya katika jimbo hilo.
Amemkabidhi gari hilo leo (Jumatano, Februari 14, 2018) mbele ya Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo, Bw. Jumaa Mhina na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Longido, Bw. Sabore ole Moloimet.
Waziri Mkuu amesema amekabidhi gari hilo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi
aliyoitoa alipofanya ziara wilayani Longidi, Agosti, 2017. Gari la kutolea
huduma za chanjo lilikuwa ni miongoni mwa changamoto zilizokuwa zinaikabili
wilaya hiyo.
Kwa upande wake, Dkt. Kiruswa alitumia fursa hiyo kumshukuru
Waziri Mkuu kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido. “Gari
hili ni zuri sana na linahimili mazingira ya wilaya ya Longido.”
“Naishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuboresha huduma
mbalimbali wilayani Longido zikiwemo za afya na maji licha ya jimbo hilo kukaa
muda mrefu bila ya kuwa na mbunge.”
Amesema atahakikisha gari hilo linatunzwa na linatumika kwa ajili ya
matumizi yaliyokusudiwa ambayo ni huduma za chanjo na afya pamoja na huduma za
mama na mtoto.
No comments:
Post a Comment