Utafiti : MATUMIZI YA Wi-Fi ,SIMU ZA MKONONI YATAJWA KUHARIBU MIMBA KWA 48%
Kukua kwa sayansi na teknolojia kumeleta WiFi inayowaruhusu watu wengi kutumia intaneti kutoka kwenye chanzo kimoja bila kuhitaji kuunganishwa na nyaya.
WiFi ni teknolojia ya mtandao inayotumia mawimbi ya redio kutoa huduma za intaneti yenye kasi kubwa. WiFi na simu za mkononi huongeza hatari ya ujauzito kuharibika mimba kwa asilimia 48, utafiti unaonyesha.
Miali ya usumaku ni mlolongo wa mawimbi ya nishati yanayosafiri kwa kasi ya mwanga inayotokana na mzunguko wa umeme wa usumaku mfano mawimbi ya redio (radio frequency), mionzi mikali ya jua (ultraviolet) au miali isiyoonekana (infrared).
Hapo zamani, watafiti wamewahi kugundua kuwa miali ya usumaku inayotolewa na minara ya simu na nyaya za umeme mkubwa husababisha msongo kwenye mwili unaoharibu chembe za urithi (jeni) tatizo linaloweza kusababisha kuharibika kwa mimba kwa wajawazito.
Miali ya usumaku ambayo kila mmoja wetu humpata kwa viwango tofauti, zamani ilihusishwa na ugonjwa wa saratani na Shirika la Afya Duniani lilipendekeza utafiti zaidi ufanyike kuona athari zake kwa wajawazito.
Watafiti wa kituo cha utafiti Kaiser kilichopo Oakland, Marekani waliwachunguza wajawazito 913 wenye mimba za umri tofauti na kugundua baadhi Wajawazito walikuwa washaharibikiwa angalau mara moja kwa vipindi vilivyopita.
Wajawazito wote walipimwa viwango vya mionzi kila siku na kifaa kijulikanacho kama Emdex Lite Meter. Watafiti walifuatilia matokeo ya kila mjamzito.
Utafiti
Watafiti waligundua wajawazito waliokuwa kwenye miali ya hali ya juu waliongeza hatari ya mimba kuharibika kwa asilimia 48 kuliko wale waliokuwa kwenye viwango vya chini.
Wajawazito waliokuwa kwenye viwango vikubwa vya miali, asilimia 24.2 waliharibikiwa mimba ikilinganishwa na asilimia 10.4 ya wale waliokuwa kwenye miali ya viwango vidogo.
Watafiti wanadai hatari hutokea bila kujali mwanamke aliwahi kuharibikiwa mimba au la. Kiongozi wa utafiti huo, Dk De-Kun Li alisema: “Utafiti huu unatoa ushahidi kwa watu kwamba miali ya usumaku huathiri afya ya binadamu kibaiolojia.”
Sababu nyingine
Nchi zilizoendelea kwenye masuala ya tiba kama Marekani wajawazito huharibika mimba kati ya asilimia 15 na 20. Nchi zinazoendelea kama Tanzania hakuna takwimu rasmi za mimba kuharibika ingawa tatizo linaweza kuwa kubwa kuliko nchi zilizoendelea.
Kitaalamu tunasema mimba imeharibika yenyewe ikiwa chini ya wiki 20 sawa na miezi mitano. Mara nyingi mimba huharibika miezi mitatu ya mwanzo ingawa mimba yaweza haribika miezi mitatu ya pili.
Mimba ikiharibika miezi mitatu ya mwanzo mara nyingi hutokana na kusababishwa na mtoto mtarajiwa. Inakadiriwa mimba nne zinazoharibika hutokea miezi mitatu ya mwanzo.
Wataalamu wanadai mimba ikiharibika miezi mitatu ya pili (kati ya wiki ya 14 na 26) basi inaweza kuwa imesababishwa na tatizo la kiafya alilonalo mjamzito. Vile vile mimba kuharibika baada ya wiki ya 26 huwa ni kwa sababu ya mfuko wa maji kupasuka kabla ya wakati kutokana na maambukizi kumzunguka mtoto. Na mara chache hutokea njia (shingo ya kizazi) inapofunguka kabla ya wakati.
Sababu za kuharibika mimba miezi mitatu ya mwanzo zinatia ndani matatizo ya kromosomu (nyuzi nyuzi katika kiini seli cha kila kiumbe ambazo hubeba viiniurithi yaani jeni), matatizo ya plasenta au kondo la nyuma.
Plasenta hupitisha lishe kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kuondosha taka za kimetaboli za mtoto. Plasenta huanza kufanya kazi kuanzia mwezi wa tatu wa ujauzito.
Vitu vinavyoongeza hatari ya kuharibika mimba ni pamoja na umri. Mmoja kati ya wanawake 10 wa chini ya miaka 30 huharibikiwa mimba Kwa wanawake wenye miaka 35 hadi 39 wanawake wawili kati ya 10 huharibikiwa mimba na kwa wanawake walio na miaka zaidi ya 45, zaidi ya nusu ya mimba zote huharibika.
Vitu vingine vinavyoongeza hatari ni pamoja na unene, uvutaji sigara wakati wa ujauzito, matumizi mabaya ya dawa mfano Ibuprofen au Misoprostol, kunywa kafeini zaidi ya miligramu 200 kwa siku, unywaji wa vileo uliokithiri zaidi ya viwango viwili vya vileo kwa wiki.
Kiwango kimoja cha kileo ni sawa na bia (lager) moja, mililita 25 za pombe kali (spirits) glasi ya mililita 125 ya divai au mvinyo ni sawa na kiwango kimoja na nusu. Sababu za kuharibika mimba miezi mitatu ya pili hujumuisha matatizo ya kiafya ya muda mrefu mfano kisukari, kupanda sana kwa shinikizo la damu, ugonjwa wa figo na magonjwa ya tezishingo (thyroid). Maambukizi ya magonjwa kama vile surua, Ukimwi, kaswende, kisonono na malaria pia husababisha mimba kuharibika.
Nyingine zinazochangia mimba kuharibika ni kula chakula chenye sumu au vyakula visivyoiva vizuri mfano nyama na mayai mabichi. Sababu nyingine ni kizazi kuwa na umbo lisilo la kawaida, kulegea kwa shingo ya kizazi na ovari kuwa kubwa kuliko kawaida hali inayosababisha mabadiliko ya homoni.
Kupunguza athari za WiFi, simu
Kuweka simu mbali na tumbo pia kutohifadhi simu kwenye mifuko ya nguo zao husaidia kupunguza athari kufika tumboni na kusababisha madhara kwa mtoto.
Inashauriwa uzime WiFi ikiwa huitumii hasa wakati umelala. Kuweka simu kwenye hali ya ndege (airplane mode) ikiwa huitumii. Kutumia waya wa sauti (speakerphone) wakati ukiongea, vilevile inashauriwa kutozungumza kwa muda mrefu.
Hivyo ni vyema kuwa mchaguzi bora wa maneno. Kutotumia vifaa vinavyotoa miali ya usumaku mfano kifaa chochote kinachotumia umeme unapokuwa kwenye gari kwa maana viwango vya miali vinakuwa juu tayari.
Fikra potofu
Kuongeza hatari ya mimba kuharibika hakuhusiani na hali ya kihisia ya mjamzito mfano kuwa na msongo au huzuni, kuwa na mshtuko kutokana na jambo fulani, kunyanyua vitu vizito, kufanya mazoezi mzazito ya viungo ingawa inapendekezwa kuwasiliana na daktari ili akupangie aina ya mazoezi ya kufanya kulingana na hali yako.
Nyingine ni kufanya kazi wakati wa ujauzito mfano kukaa au kusimama muda mrefu, kufanya ngono kipindi cha ujauzito, kusafiri kwa anga (ndege) na kula vyakula vyenye viungo vingi.
Napenda kuwatia moyo walioharibikiwa mimba kutoogopa kutafuta mimba tena baada ya mimba ya mwanzo kuharibika.
Na Dk Joachim Mabula, Mwananchi
NINI MAONI YAKO
RAIS AWASILISHA FOMU ZAKE ZENYE ORODHA YA MALI ZAKE TUME YA MAADILI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Desemba, 2017 amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasilisha fomu hiyo Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017.
“Mhe. Jaji Nsekela ikifika tarehe 31 Desemba, ambayo ni siku ya mwisho kwa Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” amesisistiza Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela amemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma sio ombi.
“Viongozi hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo na kuna sababu zake za msingi” amesema Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela.
Aidha, Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki sambamba na tamko hilo, na amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine.
Tamko la viongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni linatolewa kwa mujibu wa kifungu cha 9 na cha 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Desemba, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Desemba, 2017 amekutana kwa mara ya kwanza na kamati maalum aliyoiunda kwa lengo la kuhakiki mali za chama hicho, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kamati hiyo aliitangaza tarehe 20 Desemba, 2017 Mkoani Dodoma na inaongozwa na Dkt. Bashir Ally.
Katika Mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amewataka wajumbe wa kamati hiyo kufuatilia na kuhakiki mali zote za chama, kumhoji mtu yeyote ambaye atahitajika kutoa taarifa juu mali za chama na kubaini thamani ya mali, mahali zilipo, makusanyo ya mapato na wanaozishikilia ama kutumia mali hizo.
Mhe. Rais Magufuli pia ametoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi wengine kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zote zinazohusu mali za chama kwa kamati hiyo, na watakaoitwa kuhojiwa waitikie wito huo.
“Nataka mali za chama zikinufaishe chama, nataka mkamhoji mtu yeyote, awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote. Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, Dkt. Bashiru Ally amesema kamati imeanza kazi rasmi na ametoa wito kwa wanachama, wananchi na wote wanaozitumia mali za chama kutoa ushirikiano watakapoitwa kuhojiwa.
“Tumezungumza na Mwenyekiti kwa karibu saa mbili, katueleza matarajio yake, sababu za kuunda tume hii, kazi zake na faida zake kwa chama na kwa nchi, kwa hiyo ametukabidhi vitendea kazi na taarifa mbalimbali na ametueleza kazi yetu ni kuhakiki mali zote za chama kwa kushirikiana na wanachama na wale wanaoshirikiana na chama kuzitumia hizo mali kama vile wapangaji, wasimamizi, nakadhalika” amesema Dkt. Bashiru Ally.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Desemba, 2017
WAZIRI MWIGULU AWATAKA WANANCHI MTWARA KUJIANDIKISHA KITAMBULISHO CHA TAIFA
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba amewataka kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mtwara kushirikiana wote kwa pamoja katika zoezi la uandikishaji wa kitambulisho cha uraia ili pasiwepo na ambao si Raia wa Tanzania kuandikishwa kama Raia.
Waziri Dr Nchemba amewataka Watanzania hasa maeneo ya mipakani kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya uraia na kuwafichua wale ambao si Raia wa Tanzania ambao wamejitokeza sasa kuandikishwa ili pasiwepo baadae kesi za wasio watanzania kuandikishwa.
"Wananchi jitokezeni mtimize jukumu lenu la kujiandikisha hamnunui kitambulisho ni kutoa taarifa sahihi na zikikidhi mtapewa vitambulisho" Waziri Nchemba
Naye mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema kuwa zoezi la uandikishaji wa kitambulisho cha taifa unaendelea vizuri changamoto kubwa wanayokutana nayo ni mwitikio mdogo wa wananchi kujiandikisha huku wengi wakisingizia wanafatilia fedha zao za korosho walizouza.
WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA ZAHANATI MIBURE
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, Desemba 28, 2017. (Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Mibure, Mzee Menrad Kilian, baada ya kukagua ujenzi wa zahanati kijijini hapo, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Desemba 28, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mibure, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho Desemba 28, 2017. Waziri Mkuu yupo jimboni kwake kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa KALIF Construction, Ally Mohamed Libaba akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) wakati wakijaribu kuvuta maji kutoka kwenye pampu ya mradi wa maji wa kijiji cha Namakuku, Desemba 28, 2017. Wa kwanza kulia ni msimamizi wa mradi huo, Bw. Fadhil Ally Libaba.
*Aagiza zahanati ikiisha ipelekewe kifaa cha kutunzia watoto njiti
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, amekagua miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi kaika vijiji vya Mibure, Namakuku, Chienjere, Namahema A na Namahema B.
Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mibure jana mchana (Alhamisi, Desemba 28, 2017) mara baada ya kukagua zahanati ya kijiji hicho, Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi unavyoendelea na akamwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa ahakikishe zahanati hiyo ikikamilika inapata kifaa cha kuwatunzia watoto njiti kwa sababu kijiji hicho kiko mbali na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa.
“Nilileta makontena yenye vifaa vya hospitali, na humo ndani mlikuwa na vifaa vya kuwatunza watoto njiti (watoto wanaozaliwa kabla ya muda kutimia). Hakikisha hawa wanapata kifaa hicho kwa sababu hawana gari la kubeba wagonjwa, na pia wako mbali na hospitali ya wilaya na pia kituo cha afya cha jirani kiko mbali pia,” alisisitiza.
Akizingumzia kuhusu upatikanaji wa umeme kijiji hapo, Waziri Mkuu alisema: “Mibure ipo kwenye mipango ya kupata umeme ambao unatoka Nagurukuru, -Nghimbwa-Chienjere-Namakuku-M ibure.”
Aliwataka vijana wa kata hiyo, wachangamkie fursa kwa muanda mitaji ya kuwa na gereji za kuchomelea vyuma, saluni na viwanda vidogo vya usindikaji.
Mapema, akisoma taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Mibure mbele ya Waziri Mkuu, Mwenyeiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Chilemba alisema mradi huo umekwishagharimu sh. milioni 52, ambapo kazi zilizokamiliak ni jengo la zahanati, kichomea taka na choo chenye matundu matatu.
Alisema wanakabiliwa na changamoto ya kupanda holela kwa gharama za vifaa vya ujenzi, kupokea michango kidogo kutoka kwa wananchi, ukosefu wa nyumba ya mganga na wauguzi na kiasi cha fedha cha sh. milioni 8.26 za kununulia samani.
Bw. Chilemba alisema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia wakazi wa vijiji jirani vya Njawale, Namakuku, na vijiji jirani vya wilaya ya Nachingwea ambavyo vinapakana na wilaya ya Ruangwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 28, 2017
WANANCHI WA MKOA WA MTWARA NA MIKOA JIRANI WAMEHASWA KUTUMIA FURSA YAKIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA COMORO ILI KUIMARISHA UCHUMI
Na Gregory
Millanzi
Chama cha
Wafanyabiashara Viwanda na Kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA)wamesaini hati ya
makubaliano ya kibiashara na ushirikiano
kati ya Tanzania na Comoro kupitia Chama cha Wafanyabiashara Viwanda na
Kilimo nchini humo(UCCIA).
Hafla ya
makubaliano hayo yamefanyika mkoa hapa kwa ujumbe wenye wawakilishi saba wa
vyama vya wafanyabiashara viwanda na kilimo kutoka Comoro na visiwa vyake
vidogo vya Ngazija, Hanjuani .
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA) Swallah Said Swallah(kushoto) akiwa na Rais wa Chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo nchini Comoro (UCCIA) Ahmed Ali Bazi (kulia)
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA) Swallah Said Swallah amesema ni fursa kwa wafanyabiashra wa Mtwara kuuza bidhaa zao nchini Comoro kwani kiwango cha mauzo ya Tanzania kwa sasa ni asilimia 0.53 kiasi ambacho ni kidogo sana kulingana na ukaribu wetu, na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2020.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA) Swallah Said Swallah amesema ni fursa kwa wafanyabiashra wa Mtwara kuuza bidhaa zao nchini Comoro kwani kiwango cha mauzo ya Tanzania kwa sasa ni asilimia 0.53 kiasi ambacho ni kidogo sana kulingana na ukaribu wetu, na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2020.
Swallah
ameweka wazi mikakati ya chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara
kuhusu kuimarisha huduma za kibiashara baina ya Comoro na Tanzania na kuwaasa
wananchi kuitumia Meli mpya ambayo itaanza safari zake Januari 2018.
Naye Rais wa
Chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo nchini Comoro (UCCIA) Ahmed Ali Bazi
amesema wameamua kuja kusaini makubaliano Mkoani Mtwara kwasababu ni karibu
sana na nchi yao na kuna bidhaa nyingi ambazo wao wanazihitaji kama ambavyo
wameanza kupata cement lakini bado wanahitaji zaidi vyakulana na bidhaa zingine.
Mfanyabiashara
kutoka Mtwara Fadhiri Bashir ambae wamenunua meli kwa kushirikiana na
mfanyabiashara kutoka Comoro ili kuimarisha biashara, kwani Meli ya awali
ambayo inaendelea kufanya kazi ni ndogo ukilinganisha na huhitaji wa bidhaa
kutoka Mtwara kwenda visiwa vya Comoro na Meli hiyo itatatua tatizo la uhaba wa
usafirishaji, na itaanza kufanya kazi mwezi wa kwanza January 2018 na itafanya safari kwenda msumbiji,
Tanzania na Comoro.
Biashara baina ya nchi hizi mbili kupitia
Bandari ya Mtwara ulianza rasmi mwezi August mwaka huu na uzinduzi huo ulifanywa
na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego na pia Balozi wa Comoro
nchini Tanzania.OMOG BYE BYE SIMBA
Aliekuwa kocha Mkuu wa timu ya Simba SC Joseph Omog
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
_____________
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.
Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.
Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho,na kupumzika siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara,ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo.
Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu.
Mwisho
klabu inawatakia nyote Sikukuu njema ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.
IMETOLEWA NA....
Haji S MANARA
Mkuu wa Habari Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA
WATOTO WOTE WAPEWE ELIMU SAWA
Wananchi wa Mkoa wa Mtwara na
wilaya zake wametakiwa kuachana na mawazo mgando ya kuwabagua watoto kijinsia
katika suala la utoaji wa elimu ili kuwajengea misingi bora watoto wao.
Hayo yamesemwa na Afisa elimu,
vifaa na takwimu wa Wilaya ya Mtwara vijijini Bw. Kitonka Manase na kuwahasa
wazazi kutowanyima haki ya msingi ya kupata elimu watoto wa kike kwa sababu za
kimila na desturi.
Aidha Bw.Manase amewaomba
Wasichana waliofanikiwa katika elimu kuwasaidia wasichana ambao bado wapo kwenye
adha hii na jamii kwa ujumla kwa kuwapa elimu ili waeze kubadilika kifikra,na
kuongeza kuwa sheria haibagui jinsia,dili ,wala kabila.
Na kwa upande wake Lenfrida Mwagama Mwanafunzi wa chuo cha kilimo mkoani
Mtwara,amewashauri wasichana ambao wamepata nafasi ya kupata elimu waitumie
vizuri ili iwasaidie kujiajiri wenyewe katika maisha yao na si kuajiriwa.
Hata hivyo nchini Tanzania takwimu zinaonyesha tatizo la ubaguzi wa
kijinsia katika utoaji wa elimu kwenye miaka ya hivi karibuni kutokana na
jitahada zinazofanywa na serikali pamoja
na taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo elimu zinazoendelea kutolewa kwa
wananchi,ikiwa kwa Mwaka 2012 takwimu zinaonyesha uwiano sawa kati ya wasichana
na wavulana katika elimu ya msingi,katika elimu ya sekondari ya kawaida uwiano
ni 0.6% na sekondari ya juu ni 0.5%,hali inayoashiria kupungua kwa uwiano huo
ukilinganisha na mwaka 2017 ambapo
uandikishaji katika elimu msingi wavulana
milioni 4,629,027 sawa na 49.7% wasichana milioni 4,688,383 sawa 50.3%
katika jumla ya wanafunzi milioni 9,317,410 na kwa upande wa sekondari jumla ya
wanafunzi 199,019 wameandikishwa ikiwa wavulana 947,486 sawa 49.6% na wasichana 961,531 sawa 50.4%.
SDA YAWANOA WATOTO WA KIKE
Na Ramla Massali
Shirika lisilo la kiserikali ya Sports Development Aid ambalo limejikita katika michezo na kutoa Elimu kwa watoto wa kike, wameendelee kuwaelimisha watoto wa kike hasa wale waliopo sekondari katika kata ya mayanga.
lengo kuu ni mtoto wa kike kutambua haki zake na kuza sauti pale anapohitaji msaada. sikiliza upate kujua kile kilichijiri
Shirika lisilo la kiserikali ya Sports Development Aid ambalo limejikita katika michezo na kutoa Elimu kwa watoto wa kike, wameendelee kuwaelimisha watoto wa kike hasa wale waliopo sekondari katika kata ya mayanga.
lengo kuu ni mtoto wa kike kutambua haki zake na kuza sauti pale anapohitaji msaada. sikiliza upate kujua kile kilichijiri
Amuua Mkewe, aenda polisi na kuwaambia “Nimemmaliza nendeni mumchukue
Na Mwandishi Wetu, Kenya.
Anthony Karanja mwenye umri wa miaka 25 anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumuua mkewe kwa kumkata na shoka na kumchoma visu kufuatia ugomvi uliozuka baada ya kupokea ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake (ya Karanja).
Kwa mujibu wa Polisi wa eneo la Trans Nzoia nchini Kenya, Karanja alipokea ujumbe huo kwenye simu yake ambao mkewe aliouna na kuanzisha ugomvi kutokana na wivu wa mapenzi, lakini alijibiwa kwa kushambuliwa kwa visu na kumkata na shoka.
Polisi wameeleza kuwa mtuhumiwa ambaye alijisalimisha mwenyewe polisi baada ya kutekeleza mauaji hayo alieleza kuwa alimchoma mkewe Esther Wangui kisu kwenye paja, kwenye miguu na kifuani.
Imeelezwa kuwa baada ya kutekeleza mauaji hayo Jumapili iliyopita, alijaribu kujiua bila mafanikio na ndipo alipofika katika kituo cha polisi akipiga kelele, “Nimemmaliza endeni mumchukue.”
Majirani wameeleza kuwa walisikia ugomvi kati ya wawili hao majira ya saa moja na nusu asubuhi. Wameeleza kuwa baada ya kutekeleza mauaji, mtuhumiwa alikunywa sumu ili ajiue lakini hakufanikiwa ndipo alipoamua kujinyonga kwa kamba lakini pia hakufanikiwa.
“Mtuhumiwa aliwapeleka maafisa wetu nyumbani kwake na akawapa funguo kuwawezesha kuuchukua mwili wa marehemu,” Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Jackson Mwenga anakaririwa.
Mwenga alisema kuwa wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa na wameanza kufanya upelelezi.
FAMILIA YA BABU SEYA YAPATA PIGO
Ikiwa ni siku chache zimepita mara baada ya msanii mkongwe Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya na mwanae Papii Kocha kuachiwa huru kutokana na kupewa msamaha wa rais Magufuli katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika Desemba 9, mwaka huu mjini Dodoma familia hiyo imepata pigo baada ya mdogo wa Babu Seya aitwaye Crizo Chimbukizi kufariki dunia.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, King Kikii, Crizo alifariki dunia jana kutokana na mshtuko wa moyo baada ya kupewa taarifa ya kuachiliwa huru kwa wawili hao na kwamba taratibu za mazishi zinafanywa.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa mkoa wa Katanga Kongo nyumbani kwa familia ya Nguza.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli alitoa msamaha kwa mwanamuziki maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza maarufu kama Papii Kocha wasanii waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.
MSAADA WA KISHERIA
Na Mwandishi wetu
Naibu katibu mkuu wa wizara na sheria Amon Mpanju
ameongoza wadau mbalimbali wanaojihusisha na masula ya utoaji wa msaada wa
kisheria katika maadhimisho ya wiki ya wasaidizi wa sheria nchini, katika kanda
ya kusini
ameongoza wadau mbalimbali wanaojihusisha na masula ya utoaji wa msaada wa
kisheria katika maadhimisho ya wiki ya wasaidizi wa sheria nchini, katika kanda
ya kusini
SHERIA ZA BARABARANI ZATEKELEZWA
Madereva nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji usiozingatia sheria za barabarani.
Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania Fotunatus Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) amezungumzo pindi akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali
Kamanda Mselemu amesema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri na
Hata hivyo aliwataka wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo yatasaidia kupata sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo itakua salanma na kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria inayotekeklezeka kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50 kama
“Serikali ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali inatengeneza uchumi wa kati na viwanda kwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda miundombinu yote inayotengenezwa”
Aidha,Kamanda Mselemu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na nmapenzi ya Mungu “hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za barabarani.
Alitaja takwimu za ajali barabarani kwa Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2016 2 ilikua 639,vifo 923 na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017 kuanzia Julai hadi Septemba ajali za barabarani zilikuwa 1,376,vifo 655 pamoja na majeruhi 1,469.
Naye Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia Mery Kessy alisema zaidi ya asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni asilimia 10 tu nchi hizo zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.
Alisema wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni vijana kati ya miaka miaka 15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya afya.
CHANZO: MJENGWA