WANANCHI WA MKOA WA MTWARA NA MIKOA JIRANI WAMEHASWA KUTUMIA FURSA YAKIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA COMORO ILI KUIMARISHA UCHUMI

Na Gregory Millanzi

Chama cha Wafanyabiashara Viwanda na Kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA)wamesaini hati ya makubaliano ya kibiashara na ushirikiano  kati ya Tanzania na Comoro kupitia Chama cha Wafanyabiashara Viwanda na Kilimo nchini humo(UCCIA).

Hafla ya makubaliano hayo yamefanyika mkoa hapa kwa ujumbe wenye wawakilishi saba wa vyama vya wafanyabiashara viwanda na kilimo kutoka Comoro na visiwa vyake vidogo vya Ngazija, Hanjuani .

Mwenyekiti wa  chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA) Swallah Said Swallah(kushoto) akiwa na Rais wa Chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo nchini Comoro (UCCIA) Ahmed Ali Bazi (kulia)

Mwenyekiti wa  chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA) Swallah Said Swallah amesema ni fursa kwa wafanyabiashra wa Mtwara kuuza bidhaa zao nchini Comoro kwani kiwango cha mauzo ya Tanzania kwa sasa ni asilimia 0.53 kiasi ambacho ni kidogo sana kulingana na ukaribu wetu, na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2020.

Swallah ameweka wazi mikakati ya chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara kuhusu kuimarisha huduma za kibiashara baina ya Comoro na Tanzania na kuwaasa wananchi kuitumia Meli mpya ambayo itaanza safari zake Januari 2018.

Naye Rais wa Chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo nchini Comoro (UCCIA) Ahmed Ali Bazi amesema wameamua kuja kusaini makubaliano Mkoani Mtwara kwasababu ni karibu sana na nchi yao na kuna bidhaa nyingi ambazo wao wanazihitaji kama ambavyo wameanza kupata cement lakini bado wanahitaji zaidi vyakulana  na bidhaa zingine.

Mfanyabiashara kutoka Mtwara Fadhiri Bashir ambae wamenunua meli kwa kushirikiana na mfanyabiashara kutoka Comoro ili kuimarisha biashara, kwani Meli ya awali ambayo inaendelea kufanya kazi ni ndogo ukilinganisha na huhitaji wa bidhaa kutoka Mtwara kwenda visiwa vya Comoro na Meli hiyo itatatua tatizo la uhaba wa usafirishaji, na itaanza kufanya kazi mwezi wa kwanza January   2018 na itafanya safari kwenda msumbiji, Tanzania na Comoro.

Biashara baina ya nchi hizi mbili kupitia Bandari ya Mtwara ulianza rasmi mwezi August mwaka huu na uzinduzi huo ulifanywa na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego na pia Balozi wa Comoro nchini Tanzania.
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post