Wananchi wa Mkoa wa Mtwara na
wilaya zake wametakiwa kuachana na mawazo mgando ya kuwabagua watoto kijinsia
katika suala la utoaji wa elimu ili kuwajengea misingi bora watoto wao.
Hayo yamesemwa na Afisa elimu,
vifaa na takwimu wa Wilaya ya Mtwara vijijini Bw. Kitonka Manase na kuwahasa
wazazi kutowanyima haki ya msingi ya kupata elimu watoto wa kike kwa sababu za
kimila na desturi.
Aidha Bw.Manase amewaomba
Wasichana waliofanikiwa katika elimu kuwasaidia wasichana ambao bado wapo kwenye
adha hii na jamii kwa ujumla kwa kuwapa elimu ili waeze kubadilika kifikra,na
kuongeza kuwa sheria haibagui jinsia,dili ,wala kabila.
Na kwa upande wake Lenfrida Mwagama Mwanafunzi wa chuo cha kilimo mkoani
Mtwara,amewashauri wasichana ambao wamepata nafasi ya kupata elimu waitumie
vizuri ili iwasaidie kujiajiri wenyewe katika maisha yao na si kuajiriwa.
Hata hivyo nchini Tanzania takwimu zinaonyesha tatizo la ubaguzi wa
kijinsia katika utoaji wa elimu kwenye miaka ya hivi karibuni kutokana na
jitahada zinazofanywa na serikali pamoja
na taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo elimu zinazoendelea kutolewa kwa
wananchi,ikiwa kwa Mwaka 2012 takwimu zinaonyesha uwiano sawa kati ya wasichana
na wavulana katika elimu ya msingi,katika elimu ya sekondari ya kawaida uwiano
ni 0.6% na sekondari ya juu ni 0.5%,hali inayoashiria kupungua kwa uwiano huo
ukilinganisha na mwaka 2017 ambapo
uandikishaji katika elimu msingi wavulana
milioni 4,629,027 sawa na 49.7% wasichana milioni 4,688,383 sawa 50.3%
katika jumla ya wanafunzi milioni 9,317,410 na kwa upande wa sekondari jumla ya
wanafunzi 199,019 wameandikishwa ikiwa wavulana 947,486 sawa 49.6% na wasichana 961,531 sawa 50.4%.
No comments:
Post a Comment