Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara Mh Gelasius Byakanwa ameamuru kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya
ya Tandahimba kuwakamata viongozi wote wa vyama 35 vya msingi waliosababisha kulipa
malipo hewa kwa wakulima ambao hawajauza korosho, yenye thamani ya Shilingi Milioni 395.
Mh Byakanwa
amesema hayo wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mkoa hapa,
baada ya kukabidhiwa ripoti ya kamati ya uchunguzi wa zao la korosho Wilaya ya
Tandahimba, na kuibaini madudu mengi kwenye wilaya hiyo, na kuakikisha wote
waliohusika kuchukuliwa hatua za kisheria na mkulima mmoja mmoja analipwa pesa
yake.
Mkuu wa Mkoa
amesema, pia kamati ya uchunguzi
wamebaini takribani Bilioni 3 hazijalipwa kwa wakulima zimecheleweshwa
na wameamuru ndani ya wiki ijayo vyama hivyo viakikishe vinawalipa wakulima
wote kwa pesa zilizopo kwenye akaunti husika.
Pia Mh
Byakanwa ameamuru kamati ya ulinzi na usalama kumkamata Meneja wa Chama kikuu cha ushirika cha
Tandahimba na Newala(TANECU) Mohamed Nassoro na mtunza ghala wa chama hicho
Msafiri Zombe kutokana na upotevu korosho kwenye ghala kuu ambazo ni mali ya
vyama 5 vya ushirika ambazo ni takribani tani 194.
Kamati hiyo
ya uchunguzi wa zao la korosho Wilayani Tandahimba, iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa
ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Jackline Kasondela ambae ni Afisa Maendeleo ya
Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.
Na Gregory
Millanzi.
No comments:
Post a Comment