Walimu za shule za
Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya MASASI Mkoani MTWARA wameamua kutumia
muda wao wa likizo fupi kujengeana uwezo wa mada ngumu kwa masomo ya Sayansi,
Hisabati na Kiingereza lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi wa ufundishaji wa masomo
hayo na hivyo kuinua ufaulu katika Mitihani ya Kitaifa.
Akiongea wakati wa
mafunzo hayo katika Tarafa ya LULINDI wilayani humo, AFISA ELIMU Msingi wa
Halmashauri ya Wilaya ya MASASI Ndugu ELIZABETH MLAPONI amesema kuwa mafunzo
hayo ni kati mikakati ya kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la NNE na la SABA
kwa mwaka 2018.
Walimu wamefikia hatua hiyo baada ya kuona
baadhi ya walimu hawana uwezo wa kufundisha baadhi ya mada kutokana
kutokuzielewa vizuri hivyo mafunzo hayo yatawasaidia walimu hao kuwa na uwezo
wa kufundisha masomo hayo kwa ufanisi na hivyo kuongeza ufaulu wa masomo hayo.
MLAPONI amesema kuwa kwa matokeo ya mwaka 2017
masomo ya Kiswahili na Maarifa ya Jamii ufaulu ulikuwa asilimia 50 wakati Masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza
ufaulu ulikuwa chini ya asilimia 40 ambapo somo la Kiingereza ufaulu ulikuwa
chini ikifuatiwa na Hisabati.
Na Joina Nzali
1 comment:
Niwapongeze sana waalimu lakini pia serikali ijitahdi kuongeza walimu wa hesabu na sayansi kwani ni changamoto kubwa Sana'a kusini na masasi kwa ujumla
Post a Comment