Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma
salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kufuatia vifo vya watu 26 ambao
wamepoteza maisha katika jali ya basi dogo (Hiace) iliyogongana na Lori katika
kijiji cha Mparange Mkuranga mkoani Pwani.
Rais Magufuli ametuma salamu hizo kwa Mhandisi Evarist
Ndikilo na kumtaka amfikishe pole hizo kwa familia za watu ambao wamepoteza
maisha katika ajali hiyo mbaya iliyotokea jana tarehe 24 Machi mwaka huu.
“Nimesikitishwa sana na taarifa ya vifo
vya watu 26 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea huko
Mkuranga Mkoani Pwani, tumepoteza idadi kubwa ya Watanzania wenzetu na nguvu
kazi ya Taifa. Naungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na
majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao na watu waliowategemea”
Aidha Rais Magufuli amevitaka vyombo vinavyohusika na usalama wa
barabarani kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili
lakini pia Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema na
majeruhi 9 wa ajali hiyo wapone haraka ili waungane na familia na jamaa zao
kuendelea na shughuli za kila siku.
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment