Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo
amefunguka na kuwaomba viongozi wa CHADEMA jijini humo akiwepo Mbunge wa Arusha
Mjini Godbless Lema pamoja na Meya wa Jiji la hilo, Calist Lazaro kushirikiana
na serikali.
Mrisho Gambo amesema hayo baada ya jana Machi 24, 2018 viongozi
hao wa CHADEMA ambao anadai walikuwa wamealikwa kushiriki katika zoezi la
utoaji wa mikopo kwa kina mama kutotokea kwa kuwa zoezi hilo lilikuwa
likisimamiwa na serikali.
"Nipenda kutumia fursa hii kuwaomba
viongozi wenzangu bila kujali itikadi ya vyama vyao maana leo tulimualika hapa
mbunge, Meya na madiwani lakini wakasema tu sisi hatuendi sababu lile jambo
linasimamiwa na serikali, mimi nataka tu niwaombe viongozi wenzangu kwamba
masuala ya maendeleo hayana vyama kwa sababu na sisi pia tungeangalia vyama
pengine tungewaambia watu wa CCM wawape tu mikopo hiyo wanachama wao lakini
tukasema sisi wenye serikali watu wetu ni wote bila kujali itikadi ya vyama
vyao hivyo niwaombe wakubali kwamba Rais wa Tanzania ni Dkt. John Pombe
Magufuli"
Aidha Mkuu huyo wa mkoa amezungumzia suala la maandamano ya
April 26, 2018 kwa namna na kusema kuwa wapo watu wanafanya kazi ya kushawishi
watu kuandamana lakini wao kama viongozi wanatoa njia za watu kupambana na
maisha.
"Wakati wao wanahamasisha watu
waandamane sisi tunawapa mbinu za kupambana na maisha, wakati wao wanahamasisha
waandamane sisi tunawagea mitaji ili waweze kupata ridhiki na familia zao,
wakati wao wanahamasisha waandamane Dkt John Pombe Magufuli anatoa elimu bure
kwa shule zote nchi nzima" alisema Gambo.
Mwanadada Mange Kimambi ni kati ya watu ambao wapo mstari wa
mbele kushawishi Watanzania kote nchini kupitia mitandao ya kijamii kuandamana
April 26, 2018 ili kudai haki zao.
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment