Mkuu wa Oparesheni maalum za Kipolisi
Liberatus Sabas amesema jeshi la polisi litaendelea na ya kukabiliana na
mtandao wa dawa za kulevya Zanzibar itaendelea sambamba na kuwadhibiti wahalifu
wanaofanya vitendo vya kuwaibia na kuwadhuru watalii.
Kamanda Sabas amesema
wataendeleza operation hizo mpaka wahalifu watakaposema wamesalimu amri katika
kufanya vitendo hivyo.
Aidha amesema kwa upande wa
dawa za kulevya wamegundua wapo wafanyabiashara Zanzibar wanaoshirikiana na
wale wa Tanzania bara na kuhakikisha kwamba watawashughulikia na kisha
kuwafikisha katika mikono ya sheria na kusisitiza kuwa hakuna atakayechomoka.
Aidha imedaiwa kwatika
Oparesheni hizo wamekamatwa wahalifu wapatao 21 pamoja na kete za dawa za
kulevya kete 695 zenye ujazo takribani 31.3 gram.
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment