Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu amefunguka na kuweka wazi utata
ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na
sita na kusema taarifa ambayo inasambaa imekuwa na makosa.
Semakafu amesema hayo alipoongea na www.eatv.tv na
kusema kuwa yametokea makosa ya kiuandishi ila kujiunga na masomo ya kidato cha
tano na sita ni miaka 25 na siyo miaka 20 kama ambavyo inasomekana katika
taarifa aliyotolewa mapema leo.
"Kumetokea makosa ya kiandishi,
miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo inasomeka kwenye ile
karatasi" alisema Semakafu
CHANZO: EATV
No comments:
Post a Comment