Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa na
watanzania kwa ujumla kujenga mazoea ya kutumia bidhaa zinazozalishwa na
viwanda vilivyopo kwenye maeneo yao ili kujihakikishia soko la ndani na hatimae
kuvuka mipaka ya nchi.
Ameyasema
hayo baada ya kutembelea Kiwanda cha Unga Energy Sembe na Kiwanda cha maji Dew
Drop vinachomilikiwa na Azizi Mohamed Sudi, Mbasira Fodd Industries na Kiwanda
cha maziwa OTC Kizwite kinachomilikiwa na kikundi cha wafugaji vyote
vikipatikana katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa vinavyozalisha bidhaa
zinazouzwa ndani ya Mkoa, nje ya Mkoa na kuvuka mipaka ya nchi.
Amesema
kuwa Kazi ya Serikali kutoa mazingira bora na wezeshi ili wawekezaji wawe na
fursa nzuri za kuwekeza na kuongeza kuwa serikali haitakubali kuona viwanda
vikifa kwa mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa serikali na kuwahakikishia
wamiliki wa viwanda hao kuwa serikali haiwezi kuendelea kuhamasisha viwanda
bila ya kutatua changamoto mbalimbali zinazokumba viwanda vilivyopo.
“Tujivunie
viwanda vyetu vya hapa, hasa vile vinavyozalishwa na wazawa wenyewe ambavyo
vinatoa ajira kwa wananchi wa Mkoa huu, changamoto zipo kama masuala ya
kimazingira, malighafi na umeme, kama serikali tutayachukua ili kuhakikisha
wawekezaji wanafanya kazi katika mazingira bora kabisa, kazi ya serikali kuweka
mazingira wezeshi ili wenzetu waweke viwanda ili tuweze kufikia uchumi wa kati
wa Viwanda kufikia 2025,” Alisema.
Na
kushauri kuwa viwanda hivyo havinabudi kujitangaza katika vyombo mbalimbali vya
habari na mitandao ili kuweza kupata masoko ya uhakika.
Kwa
upande wake Mmiliki wa Kiwanda cha Unga Energy Sembe na Dew Drop, Aziz Mohamed
Sudi amesema kuwa kiwanda cha sembe kimesimama uzalishaji wake tangu Mei, 2017
baada ya kukosa soko la ndani ya nchi na kutegemewa kuanza tena mwaka 2018
baada ya kupata maombi kutoka nchi ya Kongo.
“Wawekezaji
katika mikoa ya pembezoni tumekuwa mbali na masoko makubwa, gharama za
uzalishaji, umeme na kupeleka bidhaa hizo kwenye masoko makubwa zimekuwa kubwa
pamoja na pamoja na utititiri wa kodi, hivyo tunaiomba serikali iruhusu kuuza
bidhaa za kiloimo zilizoongezwa thamani na tunakubalina na hatua za kudhibiti
chakula kwa kuuza nafaka,” Azizi Alisema.
No comments:
Post a Comment