Ligi
Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya Nane bora inataraji
kuzinduliwa rasmi mkoani Kigoma Jumapili Februari 25,2018 kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika.
Mchezo
utakaotumiwa kuzindua ligi hiyo utazikutanisha timu za Kigoma Sisterz ya Kigoma
dhidi ya Simba ya Dar es Salaam.
Aidha
uzinduzi utaenda sanjari na mpango maalumu wa FIFA wa kuhamasisha soka la
Wanawake uliopewa jina la Live Your Goal ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe.
Mbali
na mechi ya uzinduzi mechi nyingine za ligi hiyo ya Wanawake ya Serengeti
Premium Lite zinatarajia kuchezwa kesho kwenye viwanja tofauti.
Uwanja
wa Samora Panama FC watacheza dhidi ya Evergreen Queens ya Dar es Salaam saa 10
jioni,huko Mbweni JKT Queens watacheza dhidi ya Alliance saa 10 jioni,mabingwa
watetezi Mlandizi Queens wanasafiri mpaka Jamhuri Dodoma kucheza na Baobab
Queens.
Wakati
huohuo Kozi ya makocha wa kozi ya grassroots kwa watoto wenye umri wa miaka
6-12 Wasichana na Wavulana imeanza Jumatano kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika,Ujiji,Kigoma.
No comments:
Post a Comment