MAKALA: HALMSHAURI YAWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO

Image result for VIJANA MTWARALICHA ya serikali kupitia Mfuko wa kuwasaidia vijana na Wanawake kuendeleza juhudi za kuwainua Kiuchumi vijana mbalimbali,bado vijana hao wanashindwa kutumia vyema fursa hiyo

Kundi hilo la vijana ambalo linawajumuisha wanaomaliza elimu za vyuo vikuu,vijana wasiokuwa na ajira na vijana wote kwa ujumla wenye Umri (18-35) Wanaopatiwa Mikopo kiasi cha 5% kwa vijana na 5% kwa wanawake katika makusanyo ya mapato ya ndani katika halmshauri ili wajiendeleze,bado vijana wanashindwa kutumia fursa hiyo vyema na hatimaye wnabaki kuzurura na vyeti mikononi na wengine kulalamika kukosa ajira au kukosa mitaji ya biashara
Halmashauri ya Manispaa ya mtwara mikindani ni Miongoni mwa halmashauri ambazo hutoa mikopo kwa Vijana na wanawake kila mwaka

Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Manispaa hiyo imetenga shilingi milioni 487,514,287 kwa jili ya Mfuko wa wanawake na vijana (WDF) Ambayo ni sawa na asilimia 10 ya mapatao yake ya ndani na inatarajiwa kunufaisha vikundi 110

Hivi karibuni afisa maendeleo ya jamii wa halmshauri hiyo Juliana Manyama alikaririwa akisoma taarifa ya utoaji wa Mikopo alisema kuwa kwa awamu ya kwanza Jumla ya Mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 154,180,000 imetolewa kwa vikundi 48 ambavyo kati ya hivyo vya vijana ni nane peke yake

Vikundi hivyo vilivyopatiwa mikopo hujishughulisha na miradi mbalimbali ikiwemo uuzaji wa samaki,uvuvi na ufugaji 
Kati ya idadi hiyo wapo vijana kutoka Makundi mbalimbali ya waliosoma na wasiosoma na kwamba idadi ya vijana wanaojitokeza ni ndogo ukilinganisha na idadi ya vikundi vilivyopo katika manispaa hiyo

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi Beatrice Dominic anasema kuwa kati ya vijana waliopokea Mikopo hiyo wengi wanajishughulisha na shughuli za kilimo,uvuvi na shughuli nyingine za ujasiriamali ambao wanatoka katika kata mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo ya Mtwara Mikindani

Hivyo anawaasa Vijana wanaoishi katika manispaa hiyo kuitumia vyema fursa ya Mikopo inayotolewa na halamshauri hiyo,ili kukuza mitaji na kuongeza kipato na ajira,miongoni mwao na kufanya vikundi hivyo kunufaika na kutimiza Malengo ya serikali katika kukuza uchumi wa vijana nchini hususani katika halamshauri hiyo

Bi Dominiki anasema kuwa licha ya vigezo na masharti ya kupata mikopo hiyo iko wazi lakini bado vijana wanaojitokeza na kuomba mikopo hiyo idadi yake bado ni ndogo nikilinganishwa nan kundi la wanawake

Hivyo anaendelea kutoa msisisitizo kwa vijana kutumia vyema fursa hiyo,kukuza mitaji,kuongeza kipato na fursa za ajira Miongoni mwao ili waweze kujikwamua katika umaskini na kuondokana na dhana ya kutegemea kuajiriwa

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evodi Mmanda akizungumza katika hafla ya kutoa hundi kwa vikundi 48 mwanzon mwa mwezi December 2017 katika ukumbi wa Boma anasema kuwa wakati Tanzania ikielekea kwenye viwanda wajasiriamali wanatakiwa wajipange kwa ajili ya kupata ajira kwa wageni watakaokuja kujenga viwanda mtwara lakini ni fursa kwao kutengeneza bidhaa kama nguo,kupika chakula kwa mama lishe,uzoaji wa taka unaozalishwa

VIJANA WANASEMA

MWENYEKITI wa Jukwaa la vijana Manispaa ya Mtwara (MYEF)Na mwasisi wa Jukwaa hilo Salum alfati Ngauja Anasema kuwa changamoto kubwa inayowafanya vijana kutochangamkia fursa hiyo ni kutokana na vijana wenyewe Kutokuwa na utayari na wengine kuwakatisha Tamaa wale wanaoomba mikopo

Licha ya Changamoto hiyo amesema kuwa baada ya kupata Mafunzo mbalimbali yaliyowawezesha kuimarika na hadi kubuni wazo lam kuanzisha Jukwaa la kuwainua vijana Katika manispaa ya mtwara Mikindani,sasa wamebuni Mradi wa kilimo na tayari wametuma Maombi ya Mkopo katika manispaa ya Mtwara Mikindani

Amesema kuwa Kupitia Jukwaa hilo lenye zaidi ya vijana 150 wameomba kiaisi cha Takribani milioni ishirini kwa ajili ya Mradi huo na tayari wametimiza Vigezo vyote na wanatarajia kupata mkopo hivi karibuni

Hivyo anawaasa vijana wengine nchini kujaribu na Kudhubutu,bila ya kukata tamaa kuomba Mkopo Jambo litakalowasaidia kujiajiri na kuinua uchumi,pasipo kuajiriwa

Ngauja anasema kuwa Mafaniko mengi yanatokana na uvumilivu na kwamba vijana wasisubiri ajira bali wajiajiri kwa ubunifu wowote,ili wapambane na changamoto za ukosefu wa ajira,zinazowakumba vijana wengi

Anasema kuwa akiwa kijana aliamua kubuni wazo la kuanzisha jukwaa hilo ili liwe chombo cha kuwasaidia vijana kuelezea matatizo yao

Aidha amesema kuwa waliamua kubuni mradi wa Kilimo kwa kuwa wameona kuwa mradi wa Kilimo ndio unaolipa zaidi

“wengi wanashangaa vijana kufanya kilimo,ila ukweli kilimo kinalipa sana na ni kitu kitakachoweza kuleta manufaa na na kuongez uchumi”anasema Ngauja

“na kilimo tutakachofanya ni tofauti kwani tutalima mazao hasa ya mbogamboga na itakuwa ni kwa mwaka mzima hatutategemea mvua,tutafanya kilimo cha umwagiliajai”anaongeza Ngauja

Ngauja anaongeza kuwa watalima mboga za majani aina zote na viungo ikiwemo nyanya,bamia,hoho n.k

Mmoja wa vijana wa jukwaa hilo Farida abdulrahman,akisoma risala wakati wa uzinduzi wa Jukwaa hilo hivi karibuni anataja malengo ya jukwaa hilo ni pamoja na kutanua wigo wa kuwasaidia vijana wenye fani tofauti tofauti kukaa pamoja na kubadili fikra za vijana na kuondokana na dhana ya kusubiri kuajiriwa

Mtazamo wao ni kupata fedha na kuondoa kabisa hali ya umsikini miongoni mwa vijana wa halmshauri hiyo

Mmoja wa vijana hao Betina Mpinga Amesema kuwa katika mRadi huo changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa Ardhi kwani kilimo kinahitaji Ardhi kubwa kutokana pia na idadi kubwa ya vijana kuendelea kujiunga na jukwaa hilo watahitaji ardhi kubwa itakayowawezesha kufanya kilimo ambapo alitoa wito kwa halamshauri kuangalia changamoto hiyo kwa jicho la pili

Pia anasema kuwa licha ya vijana hao kujishughulisha na kilimo pia wapo vijana wengine wenyue fani mbalimbali kama udereva,upishi,ushonaji na hata upambaji hivyo kupatikana kwa mkopo kutoka halamshauri utawainua na kuwawezesha kutimiza lengo la jukwaa hilo

Vigezo vya Vijana kujiunga katika jukwaa hilo ni kijana yeyote mwenye nia ya dhati ya kupambana na umaskin anayeishi ndani ya manispaa ya Mtwara mikindani.

Na John Massawe - Jamii Fm Radio
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post