ACT WAZALENDO NA UJUMBE WA BARAZA LA MAASKOFU


Chama cha ACT-Wazalendo, kimesema ujumbe wa Kwaresma mwaka 2018 uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuhusu masuala  ya kisiasa, kichumi na kijamii unaonyesha jinsi demokrasia inavyominywa nchini.
TEC imetoa ujumbe huo Februari, 2018 ulioandikwa na maaskofu wote 35 wa baraza hilo, wakiongozwa na Rais wake, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa upo katika kitabu cha kurasa 20 ikiwa ni maandalizi ya ibada ya siku 40, kipindi ambacho ni cha mfungo wa kukumbuka siku 40 za Kristo kufunga na kwenda jangwani.
Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu amesema, “Tunawapongeza  sana viongozi wetu wa dini kwa kujitokeza waziwazi kuonyesha ugandamizaji wa haki unaoendelea nchini.”

“TEC kutoa waraka wa kiuchungaji ni kurasa mpya katika siasa zetu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike.” Katika ujumbe huo,  TEC wamezungumzia hali ya kisiasa na kusema uamuzi wa Serikali kuzuia, maandamano, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni kwenda kinyume cha Katiba ya nchi.
Shaibu ameitaka Srikali kuondoa zuio batili la vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara ya kuzungumza na wananchi.
 Mbali na hilo, Shaibu ameiomba Serikali itoe taarifa ya uchunguzi kupotea kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Azory  Gwanda aliyefikisha siku 84 tangu kupotea kwake sanjari na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo, Simon  Kanguye.

Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post