• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

MTWARA: "Ni Marufuku matumizi ya Msumeno wa Mnyonyoro (chainsaw)"


Serikali ya wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara imepiga marufuku matumizi ya msumeno wa Mnyonyoro(chainsaw)ambayo inadaiwa kuwa chanzo cha uvunaji holela wa miti Wilayani humo. 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Mtwara,Evod Mmanda wakati akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la upandaji wa Miti katika wilaya hiyo ambapo pia amezitaka halmashauri zote katika wilaya ya Mtwara kuzuia na kudhibiti uvunaji holela wa miti kwani hali hiyo inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

"Mtu anayemiliki Chainsaw hana tofaut na mtu anayemiliki mtambo wa gongo" alisema Mmanda na kulngezea "utaratibu wa kuvuna miti unafahamika lazima uombe kibali kuanzia ngazi ya kijiji na kijiji waandike muhtsari walete wilayani hata kama ni mwembe wako lazima ufuate utaratibu huo"  Mmanda amesema

kuwa utaratibu huo si wake bali utaratibu wa kisheria na hivyo atakayekiuka atachukuliwa hatua Kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.  Awali kaimu katibu tawala wa Wilaya ya Mtwara,Fransis Mkuti akisoma taarifa ya upandaji miti katika wilaya hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2017 had machi mwaka huu amesema kuwa jumla ya miti 594876 imepandwa.

John G Massawe,Jamii FM
Share:

MTWARA: MKUU WA MKOA ATANGAZA KIAMA KWA WALE WOTE WANAOHUJUMU ZAO LA KOROSHO MKOANI HUMO


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh Gelasius Byakanwa ameamuru kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Tandahimba kuwakamata viongozi wote wa vyama 35 vya msingi waliosababisha kulipa malipo hewa kwa wakulima ambao hawajauza korosho, yenye  thamani ya Shilingi Milioni 395.

Mh Byakanwa amesema hayo wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mkoa hapa, baada ya kukabidhiwa ripoti ya kamati ya uchunguzi wa zao la korosho Wilaya ya Tandahimba, na kuibaini madudu mengi kwenye wilaya hiyo, na kuakikisha wote waliohusika kuchukuliwa hatua za kisheria na mkulima mmoja mmoja analipwa pesa yake.

Mkuu wa Mkoa amesema, pia kamati ya uchunguzi  wamebaini takribani Bilioni 3 hazijalipwa kwa wakulima zimecheleweshwa na wameamuru ndani ya wiki ijayo vyama hivyo viakikishe vinawalipa wakulima wote kwa pesa zilizopo kwenye akaunti husika.

Pia Mh Byakanwa ameamuru kamati ya ulinzi na usalama kumkamata  Meneja wa Chama kikuu cha ushirika cha Tandahimba na Newala(TANECU) Mohamed Nassoro na mtunza ghala wa chama hicho Msafiri Zombe kutokana na upotevu korosho kwenye ghala kuu ambazo ni mali ya vyama 5 vya ushirika ambazo ni takribani tani 194.

Kamati hiyo ya uchunguzi wa zao la korosho Wilayani Tandahimba, iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Jackline Kasondela ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba.

Na Gregory Millanzi.



Share:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post