DODOMA
Waandishi wa habari wanawake nchini wametakiwa kutumia uwezo wao kitaaluma wanapotekeleza majukumu yao badala ya kutegemea upendeleo kutoka kwa waajiri wao.
Baadhi
ya wanawake wamekuwa wakijiingiza katika masuala ya mapenzi kwa mategemeo ya
kupandishwa vyeo au kupata upendeleo badala ya kutumia uwezo walio nao
kitaaluma jambo ambao linawashushia hadhi na heshima mahali pa kazi.
Waandishi wa habari kutoka Redio za Jamii Tanzania wakiendelea na mafunzo |
Hayo
yamesemwa na Mkufunzi wa Redio za Kijamii
nchini kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO - Bi
ROSE MWALIMU katika semina inayoendelea katika Ukumbi wa Wakala wa Majengo mjini DODOMA ya kuwajengea uwezo waandishi wa
habari za kijamii kutoka vituo 24 vya redio za kijamii nchini kuhusu uandaaji
wa habari na vipidi bora.
Akiwasilisha
mada inayohusu maadili ya vyombo vya habari kwa washiriki wa semina hiyo Bi ROSE
amesema wazazi na walezi wamewasomesha
watoto wao ili kuwapa uwezo na kuwajenga kitaaluma kwa lengo la kulitumikia
taifa kiuadilifu pamoja na kujipatia kipato cha kujikimu na maisha.
Amesema
badala yake waandishi wengi wanawake wamekuwa wakishindwa kutumia elimu
waliyoipata katika utendaji wao wa kazi na wamekuwa wakidanyanyika kwa kufanya
mapenzi na waajiri wao kwa lengo la kujinufaisha kwa kipato na upendeleo
mbadala.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe anatarajia kuhudhuria maadhimisho ya siku ya redio duniani |
Wakichangia
mada hiyo baadhi ya washiriki wa semina wamesema wanawake wengi hushindwa
kufanya kazi zao kiuadilifu kutokana na tamaa
za maisha na kipato kidogo wanachopewa na waajiri na wakati mwigine
kukosekana kabisa.
Mafunzo
hayo ya siku nane yatahitimishwa tarehe 13/2/2018 ambapo maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yataadhimishwa mjini DODOMA na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dr. HARRISON MWAKYEMBE anatarajia kuhudhuria hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment