SIMON GROUP YACHANGIA MILIONI 25 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU

PICHA TA TATUKampuni ya Simon Group imechangia kiasi cha Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu  katika mkoa wa Simiyu
Akikabidhi hundi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Simon Group, Ndg. Leonard Kitwala amesema  Kampuni hiyo imetoa fedha hizo ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya Sekta ya Elimu na kwa kuwa Simiyu ni mahali alipozaliwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Simon Kisena ameona ni vema  asaidie maendeleo ya elimu nyumbani kwao.

Aidha, Kitwala amesema kama kampuni wameamua kuunga mkono ujenzi wa miundombinu ya Elimu Simiyu kwa kuwa wamependezwa na juhudi za Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kuwaletea maendeleo wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu.

Akipokea hundi ya shilingi milioni 25 kwa niaba ya Viongozi na wanafunzi wa  Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka amesema anaishukuru Kampuni ya Saimon Group ambayo inaendesha mradi wa Usafrishaji wa Mabasi Dar es Salaam(UDA) kwa kuamua kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu mkoani humo.

“Nawashukuru sana SAIMON GROUP kwa kuamua kusaidia ujenzi wa miundombinu ya elimu Simiyu, shilingi milioni 25 ni fedha nyingi sana kwenye kufanikisha ujenzi wa mundombinu ya elimu  hasa kwa mkoa kama wa kwetu ambao shughuli nyingi za ujenzi tunatumia “Force Account” , tunatumia nguvu za wananchi na Serikali ina nafasi yake  katika ujenzi wa miradi hiyo” alisema.

“Zaidi sana namshukuru Mkurugenzi wa SIMON GROUP ndugu Robert Kisena ambaye ni  mzaliwa  wa Mkoa huu kwa kuona arudishe sehemu ya faida ya biashara zake nyumbani, kwa niaba ya viongozi wenzangu ninamkikishia kwamba mchango huu utaenda kwenye matokeo yanayoonekana, hata wakati wa uzinduzi wa madarasa yatakayojengwa tutaipa  nafasi Kampuni ya SIMON GROUP kuja kuona alama waliyoweka katika mkoa wetu” alisisitiza Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe.Robert Lweyo amesema mchango huo wa SIMON GROUP umekuja katika muda muafaka ambao mkoa huo una uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa hivyo alimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Robert Kisena na kuahidi pia kuwa fedha hizo zitafanya kazi iliyokusudiwa.


Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post