Wafanyabiashara
wa mazao ya Misitu hasa Mkaa, Kuni na Mbao wilayani MASASI wametakiwa kufuata sheria
wakati wa kuvuna mazao hayo kwa kupata
vibali vitakavyowawezesha kufanya biashara hiyo
Akizungumza na wananchi
wakati wa ziara ya kutoa elimu juu ya sheria zinazotakiwa kufuatwa, AFISA
MISITU MBWANA MILANZI amesema kuwa idara ya misitu inapita kutoa elimu juu ya
sheria na taratibu za kufanya biashara ya misitu kwa mara ya mwisho na baada ya
Elimu hii sheria itafuata mkondo wake.
MILLANZI amefafanua kuwa "Sio
mara ya Kwanza kwa wakala wa misitu wilani Masasi kutoa elimu hii kwa wananchi,
hivyo watu wanafahamu ndio maana wakikutana na watu wa maliasili wanakimbia.
Hivyo kwa anayetaka kuendelea kufanya biashara ya misitu ni lazima afuate
sheria ili kulipa kodi ya serikali na kulinda misitu yetu ambayo ina faida kubwa
kwa maisha ya binadamu".
Kutokana na
changamoto hiyo Wakala wa Misitu Wilayani MASASI inawakumbusha wafanyabiashara
wote kutambua sheria na kanuni zilizowekwa na idara hiyo ili waweze kutambulika
lakini pia kuzuia uvunaji holela wa mazao Hayo hali inayopelekea uharibifu
mkubwa wa
misitu.
No comments:
Post a Comment