Viongozi wanne wa Chadema wamewasili Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu Dk vicenti Mashinji.
Viongozi hao ambao wamewasili Polisi kwa ajili ya kuitikia wito ni pamoja na manaibu katibu John Mnyika na Salum Mwalimu pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti John Heche.
Wakili wao Fredrick Khiwelo amesema wengine wako njiani akiwamo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikaeli Mbowe.
Awali Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai kwa Taifa Leo tarehe 22 Machi 2018, ametoa waraka wa kuitwa Polisi yeye na viongozi wenzake.
Katika waraka huo Mbowe amesema kwamba kuna taarifa pia ya kumuunganisha Peter Msigwa, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika shauri hili.
Updates: Mbowe, Mwalimu Wameachiwa Kwa Dhamana......, Heche na Mnyika washikiliwa, Mdee na Matiko wanasakwa..
Viongozi watatu wa Chadema walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji wameachiwa kwa dhamana huku wawili wakitakiwa kubaki.
Viongozi walioachiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk Mashinji.
Mwalimu amesema Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wamebaki polisi kwa maelezo kuwa wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.
Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 huku chama hicho kikieleza kuwa moja ya sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.
Dk Mashinji ameeleza kuwa viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa kuripoti polisi leo akiwemo mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamepata dharura.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
No comments:
Post a Comment