# Kifua Kikuu(TB) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani.
# Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua Kifua Kikuu kila mwaka Duniani na Milioni Moja kati ya hao ni watoto wenye umri chini ya miaka 15.
# Tafiti nyingi zinaonesha kuwa karibia theluthi moja ya Watanzania tayari wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu na wanaishi na vimelea mwilini mwao.
# Kauli mbiu ya mwaka huu inasema *” Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB.”*
#Nchini Tanzania kila mwaka jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu.
# Nitoe wito kwa viongozi wa ngazi zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele.
# Napenda kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa zake zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo vya Umma na Binafsi.
# Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua Kikuu nchini ikiwemo kuimarisha uchunguzi na ugunduzi wa Kifua Kikuu katika Vituo vya Afya.
# Serikali na wadau mbalimbali tunaendelea na utekelezaji wa kampeni za uhamasishaji na upimaji wa Wananchi katika maeneo ya migodi, makazi duni kwenye miji mikubwa, magereza na shule za bweni.
# Pia Serikali imezindua dawa mpya za TB za watoto ili kuhakikisha zinakidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani ( WHO), dawa hizo mpya ni za watoto za mseto ( RHZ/RH) zilizoboreshwa na tayari zimeshawasili nchini na tumeanza kuzisambaza kwenda Mikoani na Halmashauri zote nchini.
# Nawaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya kuanza masomo.
#Ni marufuku kwa Madaktari kujaza fomu za uchunguzi wa Afya bila kupima wanafunzi husika. Kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika.
# Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB.
#Mpaka sasa takribani watoa huduma1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu wanawezeshwa ili kuibua wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment