Rais John Magufuli amewataka wafanyabiashara wenye madeni sugu ya kodi kufanya mazungumzo na Wizara ya Fedha pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili waweze kupata punguzo la madeni wanayodaiwa.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo katika Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara, uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dkt. Magufuli amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango kuwangalia wafanyabiashara hao kwa jicho la kibinadamu na kwamba asipotumia njia hiyo wafanyabishara hao wanaweza kufilisika iwapo watalipisha ffedha zote wanazodaiwa.
“Mnaodaiwa kwa miaka ya nyuma nendeni mkazungumze na wizara ya fedha, najua kuna kipengele kinaweza kuwapunguzia, wapo watu wanadaiwa zaidi ya bilioni 400, waziri wa fedha muwe na human ground la sivyo mtawafilisi wafanyabiashara, mkiwafilisi mtakusanya wapi kodi, Nawaachia wizara ya fedha na TRA muliangalie hili” amesema na kuongeza.
Katika hatua nyinge, Rais Magufuli ameiagiza TRA kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kodi ili kuwavutia wafanyabiashara, huku akiwataka wafanyabiashara hao kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
“Nilizungumza na watendaji wa TRA na wizara ya fedha, TRA niliwambia tunategemea wafanyabisahara ikitokea umewavuruga utakusanya wapi kodi, inatakiwa ujenge mazingira ya kuwavutia wafanyabiashara.”
No comments:
Post a Comment